Na Lango La Habari
Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam limemkamata GADI DAUDI maarufu tito Jeshi la mtu mmoja (28) Mkazi wa Ubungo Riverside kwa tuhuma za kumuua JULIUS FREDRICK (22) Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kumpora simu yake ya mkononi .
Kupitia taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam ACP Jumanne Muliro amesema Tukio hilo lilitokea tarehe Julai 16, 2022 majira ya saa kumi usiku karibu na hosteli za Magufuli Wilaya ya Ubungo Dar es Salaam ambapo Gadi alimvizia Julius na kumpora vitu kisha kumshambulia na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili hali iliyomsababishia kifo.
Kamanda Muliro amesema Jeshi la Polisi lilifanya upelelezi na ufuatiliaji wa kina ambapo Julai 27, 2022 lilifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo maeneo ya Sinza, Kinondoni.
"baada ya kumuhoji kwa kina alikiri kumuua mwanafunzi huyo na kumpora vitu vyake na alikiri pia kufanya matukio kama hayo ya unyanganyi kwenye maeneo tofauti ya jiji la Dar es Salaam" ameelezea Kamanda Muliro
Amesema baada ya uchunguzi kufanyika Jeshi la Polisi lilibaini kuwa mtuhumiwa huyo ni mhalifu sugu ambaye amekuwa akifanya matukio katika maeneo ya Mlimani city, Mwenge na Kawe.

Pia mtuhumiwa huyo aliwahi kushtakiwa kwa kesi ya UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA kesi No. 256/2020 na kufungwa miaka 30 kuanzia Julai 06, 2020 na aliachiwa huru Aprili 2022 kwa sababu za kisheria baada ya kukata rufaa.
Mnamo August Mosi, 2022 majira ya saa kumi na nusu jioni Mtuhumiwa alikubali kuwapekeleka askari kuwaonesha alipoficha silaha anazotumia katika uhalifu na simu ya marehemu aliyoipora katika vichaka vilivyopo eneo la katikati ya Mlimani city na Hostel za Magufuli.
Baada ya kufika eneo hilo alikurupuka na kuanza kukimbia kuelekea kwenye vichaka vya ndani zaidi Askari walifyatua risasi tatu hewani kumtahadharisha kusimama lakini alikaidi na hivyo kulazimika kumzuia kwa risasi iliyomjeruhi kwenye paja la mguu wa kushoto, kuanguka chini na kukamatwa kutoka katika jaribio la kutoroka chini ya ulinzi huku akikabiliana na tuhuma nzito za mauaji .
"Alipelekwa hospitali kwa matibabu. Eneo hilo Polisi imepata panga moja, sime, bisibisi na simu mbili za mkononi" Kamanda Muliro
Aidha Kamanda Muliro ameongeza kuwa la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam liendelea na msako mkali kuwakamata wahalifu wote wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu na malengo ni kuhakikisha watu wanafanya shughuli zao katika mazingira yaliyo salama , bila hofu na kwa kuzingatia sheria za nchi.