OR-TAMISEMI
Kikundi cha vijana nane wamefungua mradi wa Zahanati baada ya kupatiwa mkopo wa Sh.milioni 110 uliotokana na mapato ya asilimia 10 ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Kati ya vijana hao, wapo Madaktari wawili, Mfamasia mmoja, Wataalam wa maabara wawili, Wauguzi wawili na Mwanasheria mmoja ambapo wameanzisha mradi huo kwenye eneo la kipunguni kwa Mkolemba na kuzinduliwa rasmi jana na Mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Mbunge Silaa amewapongeza vijana hao kwa hatua hiyo ambayo ni mfano wa kuigwa kwa kuwa badala ya kutafuta ajira wametoa ajira.
“Nimepewa ulezi, nitawalea kwa moyo na kuhakikisha wamekua, huu ni mfano halisi wa kazi kubwa ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwatengenezea vijana mazingira ya kujiajiri Mikopo ya Halmashauri inalipa jiongeze kuwa mbunifu,”amesema.