Tuesday, 16 August 2022

MAMBA AUA MWANAMKE ALIYEKUWA AKICHOTA MAJI MTONI




Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Orester Haule (25) mkazi wa kijiji cha Kipingu Halmashauri ya wilaya ya Ludewa mkoani Njombe amefariki dunia baada ya kukamatwa na mamba na kumzamisha kwenye Maji wakati akichota maji katika mto Ruhuhu kwa ajili ya matumizi ya nyumbani

Mama huyo ameacha watoto wawili wadogo

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Kipingu Alphonce Mbeya anasema tukio hilo limetokea Agosti 13 majira ya saa 12 jioni wakati mwanamke huyo akiwa na wenzake wakifata huduma ya maji kwa matumizi ya nyumbani ambapo inaelezwa hadi tukio hilo limetokea tayari watu 4 wameshambuliwa na mamba wakisaka maji

Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Ludewa wamelazimika kufika msibani kuwapa pole wafiwa na kisha kuahidi kutatua changamoto ya mradi wa maji katika kijiji hicho huku pia wakitoa agizo kwa wizara ya mali asili na utili kuwavuna mamba katika mto huo ili kunusuru vifo vinavyoweza kuzuilika.


Source: EATV

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages