Breaking

Wednesday, 24 August 2022

MAMA NA WATOTO WATANO WANUSURIKA KUUAWA MANYARA




Mariamu Ramadhani na watoto wake 5 wakazi wa wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, wamenusurika kuuawa na mtalaka wake walioachana miaka 17 iliyopita.

Inaelezwa kuwa mwanaume huyo alifika nyumbani kwa mwanamke huyo akiwa na Panga, Kisu na Sururu ambapo mwanamke aliamua kukimbia kabla ya mwanaume huyo kuanza kubomoa nyumba na kuiba baadhi ya mali

Baadhi ya mashuhuda wameliomba Jeshi la Polisi Kiteto kufuatilia tukio hilo ili liwe fundisho pamoja na kwamba vitendo vya ukatili Kiteto vimetajwa kukithiri.

Hata hivyo baada ya mtalaka huyo kutoweka katika mazingira hayo mwanaume huyo aliishia kubomoa nyumba kisha kuingia ndani na kuchukua fedha taslimu shilingi laki mbili za mtalaka na kutoweka kusikojulikana.


Source: Eatv
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages