Breaking

Wednesday, 17 August 2022

DED KISHAPU AWATAKA WAFANYABIASHARA KULIPA KODI, KUSHIRIKIANA



Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya kishapu, Emmanuel Johnson amewataka wafanyabiashara kuwa wamoja na kujenga mshikamano katika kukuza maendeleo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu.

Johnson ameyasema hayo alipokutana na wafanya biashara katika mji mdogo wa Maganzo uliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga.

Amesema lengo la kukutana na wafanyabiashara hao ni kufahamiana ili kuwaunganisha na kuwalezea taratibu na sheria ili waweze kuendesha biashara zao bila usumbufu wowote pamoja na kujua fursa zilizopo katika Halmashauri hiyo.

Amewasa wafanyabiashara kushiriki kikamilifu katika ulipaji wa kodi hali itakayochochea maendeleoya nchi na kuijenga Halmashauri na wilaya ya kishapu.

"wafanyabiashara wanawaona TRA Kama maadui lakini kwa utaratibu TRA ni rafiki yako kwa sababu tunasema (TRA KWA PAMOJA TUJENGE NCHI YETU)" Amesema Mkurugenzi Johnson

DED. Johnson ameeleza umuhimu na faida ya kulipa kodi pamoja na mgawanyo wa kodi hizo ndani ya halmashauri ya wilaya ya Kishapu.

“Nataka tufahamu kodi tunazolipa sisi wananchi wa Kishapu moja hapa tunao wafanya biashara wakina mama na Vijana kupitia kodi tunazo zikusanya kwa wananchi tunapata mapato y ndani ampapo asilimia 10 inatengwa kwajili ya mikopo isiyokuwa na riba kwajili ya akina mama, vijana na watu wenye ulemavu” alisema Mkurugenzi

Aidha mkurugenzi alihimiza swala la Sensa ya watu na makazi kwa kuwataka wananchi kutoa ushirikiano wa kutoa taaria zilizo sahihi kwa makarani wa Sensa na kuwaeleza mikakati ya Serikali kupitia sensa ya watu na Makazi ni pamoja na kupanga bajeti ya kuu ya Serikali kwa watu wake.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages