Breaking

Wednesday, 31 August 2022

WANAFUNZI SABA WAKAMATWA TUHUMA ZA KUCHOMA BWENI


Polisi katika Kaunti ya Homa Bay wanawazuilia wanafunzi saba kwa tuhuma za kuhusika katika mkasa wa moto katika Shule ya Upili ya Ober Boys katika kaunti ndogo ya Rachuonyo Mashariki Nchini Kenya.

Saba hao wanatuhumiwa kuteketeza bweni siku ya Jumatatu August 29, 2022 majira ya asubuhi wenzao wakiwa darasani ambapo moto uliteketeza bweni lenye uwezo wa kusheheni wanafunzi 167.

Mmoja wao alikiri kuhusika katika kisa hicho cha alfajiri.

Wanafunzi waliokuwa darasani na kuona moshi ukitoka kwenye bweni hilo walipiga kamsa.

Wazima moto kutoka Serikali ya Kaunti ya Homa Bay walifanikiwa kuuzima moto huo kabla ya kusambaa hadi majengo mengine. Hata hivyo mali ya thamai isiyojulikana ilibaki kuwa jivu.

Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Homa Bay Samson Ole Kinne anasema kuwa wafunzi hao saba walioshikwa wanaaminika kuwa nyuma ya kisa hicho cha moto shuleni.

Kwa mujibu wa Ile Kinne, wanafunzi hao walipelekea katika kituo cha polisi cha Ringa na baada ya kuhojiwa mmoja wao ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili alikiri kuhusika.

Wanafunzi hao wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Ringa huku uchunguzi ukiendelea. Hakuna aliyejeruhiwa katika kisa hicho kwani wanafunzi wote walikuwa darasani.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages