Breaking

Thursday, 18 August 2022

WANAOPANGA KUVURUGA ZOEZI LA SENSA WAONYWA



Mbunge wa Jimbo la Sengerema Tabasam Hamis amewaonya wananchi ambao watadiriki kuvuruga zoezi la Sensa ya watu na Makazi siku ya Agosti 23 mwaka huu huku akiwaomba watendaji wa kata huska kuchukua hatua kali kwa yoyote yule atakae jaribu kuaribu zoezi hilo.

Kauli hiyo imetolewa na mbunge wa Sengerema Tabasam Hamis katika kijiji cha Buzilasoga kata ya Buzilasoga wilayani humo mkoani Mwanza kwenye mkutano wa hadhara wenye lengo la wakati kutoa elimu juu ya zoezi la kushiriki Sensa ya Watu na Makazi.


Kwa upande wake Afisa mipango wa halmashauri ya wilaya ya Sengerema mkoani humo,Pastory Mkaruka,akawataka wananchi wa kata ya hiyo kutoa ushirikiano kwa Makarani wa Sensa siku ya zoezi hilo linarotarajiwa kufanyika Agosti 23,mwaka huu.

" Wakazi wa kijiji cha Buzilasoga kata ya Buzilasoga halmshauri ya Sengerema, wakizungumza katika mkutano huo wamesema ,wao wako teali kushiriki na kuhesabiwa katika zoezi la Sensa ya watu na Makazi Agosti 23 kwakua zoezi hilo litaleta manufaa makubwa kwa upande wao baada ya serikali kujua idadi yao harisi

Naye Diwani wa kata ya Ibondo wilayani humo,Mathias Mashauri amesema,katika kata hiyo ambayo ni miongoni mwa kata za wilaya ya Sengerema wananchi wamekuwa na mwitikio mkubwa kuhusiana na zoezi la Sensa ya watu na Makazi kutokana huu akisema kuwa, ni haki ya kila mtanzania kuhesabiwa.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages