Breaking

Tuesday, 16 August 2022

RC TABORA AWATAKA WAKULIMA KUJISAJILI KUPATA MBOLEA YA RUZUKU



Na Lucas Raphael,Tabora

Mkuu wa Mkoa Tabora Balozi Dkt. Batilda Burian amewataka wakulima kujisajili katika ofisi za Serikali za Mitaa/Vijiji ili waweze kunufaika na mbolea za ruzuku inayotolewa na serikali kwa ajili ya msimu wa kilimo wa 2022/2023.

Rc Dkt. Batilda ametoa wito huo leo Jumanne August 16, 2022 alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tabora.

Amesema kwamba mara baada ya wakulima wakishajisajili watapata namba ya utambulisho ambayo itatumika kununua mbolea kwa bei ya ruzuku, bila kufanya hivyo hawataweza kunufaika na mbolea hizo.

Alisema kwamba kwa wananchi wa Mkoa wa Tabora naomba wanampongeze Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuwa na dhamira njema ya kuwasiadia wakulima wa nchi hii.

Alisema kwamba serikali imeweza kushusha bei ya mbolea kwa wastani wa kati ya 39.7% na 46.8%.

Balozi Dkt. Batilda alisema kwamba mbole ya DAP iliyokuwa ikiuzwa kwa wastani wa shilingi 131,676 sasa itauzwa kwa wastani wa 70,000 kwa mfuko wa kilo 50 na hiyo ndio Wastani wa bei ya mbolea kwa mfuko wa kilo 50 kwa sasa

Mbole aina ya urea iliyokuwa inaunzwa kwa shilingi 124,724 na sasa itanunuliwa kwa beei ya Ruzuku 70,000,Can iliyokuwa inaunzwa kwa shilingi 108,156 kwa bei ya Ruzuku itanunuliwa shilingi 60,000/.

Alisema kwamba mbolea ya SA ilikuwa inaunzwa kwa shilingi 82,852 sasa itanunuliwa kwa bei ya Ruzuku kwa shilingi 50,000 na Npk ilikuwa inanunuliwa kwa shilingi 122,695 sasa kwa bie ya ruzuku itakuwa ni shilingi 70,000.

Alisema kwamba Tayari nimeisha toa maelekezo kwa Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Maafisa Kilimo na Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji kulisimamia zoezi hili la Usajili.

“Rais ametutaka kusimamia kikamilifu zoezi la utoaji wa mbolea za ruzuku ili ziweze kuwafikia wakulima na kuleta tija ya uzalishaji wa mazao ya kilimo”.alisema Balozi Dkt. Batilda

Katika mwaka fedha wa 2022/2023, Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 150 kugharamia ruzuku ya mbolea itakayotolewa kwa wakulima wa mazao yote nchini kwa lengo la kupunguza makali ya bei ya mbolea.

Lengo kubwa la kutoa ruzuku hiyo ni kuongeza uzalishaji na tija katika kilimo, kuimarisha usalama wa chakula na kuongeza upatikanaji wa malighafi za viwanda vya ndani.


Mwisho
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages