Breaking

Monday, 29 August 2022

KOCHA TAIFA STARS ATIMULIWA



Na Said Muhibu,

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemuondoa Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Kim Poulsen kuiona timu hiyo baada kukaa kikao cha pamoja kwa pande zote mbili.

TFF imesema Poulsen na wasaidizi wake wameondolewa kwenye benchi la ufundi la Taifa Stars na kuongeza kuwa atabaki katika Timu za Taifa za vijana mpaka mkataba wake utakapomalizika.

Benchi la ufundi la Taifa Stars litakuwa chini ya Kocha Hanour Janza akisaidiwa na Meck Maxime na Kocha wa magolikipa Juma Kaseja.

Poulsen raia wa Denmark aliwahi kuhudumu ndani ya kikosi cha timu ya taifa ya wakubwa na wadogo kabla ya kumaliza kazi hapa nchini akiwa kama mkurugenzi wa benchi la ufundi Serengeti Boys.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages