Mkuu wa wa Wilaya ya Kishapu Mhe Joseph Modest Mkude amekabidhi trekta aina ya SWARAJ 855 FE kwenye kikundi cha AMCOS Cha kijiji cha Kishapu kilichopo Halmashauri ya wilaya ya Kishapu.
Trekta hiyo yenye thamani ya million 40 iliyonunuliwa Na kikundi kutokana na ushuru wa Choroko na mkopo wa millioni13 kutoka katika BANK ya NMB ikabidhiwa Jumanne Agusti 16, 2022 mbele ya ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu.
Dc Mkude amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kwa kusimamia vyema Saccos na Amcos pamoja na kushirikiana na Bank ya NMB kuhakikisha wanakikundi hao wanapata trekta hiyo ambayo itawasaidia kukua kiuchumi na kuchochea maendeleo ya Wilaya.
Amewaasa wanakikundi kuitunza na kuwa na ufuatiliaji wa karibu na kuhakikisha wanaifanyia matengenezo ya kina pale inapopata hitilafu yoyote.
"hatuwezi kuwa na uchumi imara bila kuwa na Nyenzo za kuzalishia Mali sisi asilimia kubwa sisi ni wakulima wakulima tunahitajinyenzo hizi kama trekta na zingine ili zitusaidie katika kujikwamua kiuchumi “ Dc Mkude alizungumza
Aidha Dc Mkude ameagiza usimamizi mzuri kutoka kwa wataalamu wa ngazi ya Halmashuri na kutoa onyo kwa wale wote watakao thubutu katika ubadhilifu wa mali za umma.
Kwa upande wake katibu Tawala wilaya ya Kishapu, Shadarack Kengese amewapongeza AMCOS ya Kiiji cha Kishapu kwa kuonyesha dhamira nzuri na kuonyesha mfano mzuri kwa AMCOS zingine na kuwataka wanakikundi wawe na na mshikamano katika utunzaji
“wanakikundi wameonyesha nia ya dhati kabisa kwa maana inawezekana kwa hiyo AMCOS zingine ziige kutoka kwenye AMCOS ya Kishapu, nyingi zinapata mapato mengi lakini ukijiuliza wanafanya nini hupata majibu ya kulidhisha kuna baadhi za AMCOS hata kilichopo wanatamani wakigawane, niwapongeze sana kwa kununua Trekta kwa hiyo Idara husika wasimamie ipasavyo." Amesema Das Kengese
Naye Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Emmanuel Johnson Ametoa shukurani na kukipongeza kikundi cha AMCOS kilichopo kijiji cha Kishapu kwa kutoa mfano mzuri na kuwaeleza dhamira ya sasa ya Serikali kwa sasa ni kilimo biashara.
“natoa wito kwa AMCOS zingine ni vizuri zikafikilia kipi cha kufanya na dhamira ya Serikali kwa sasa ni kilimo biashara, Kilimo biashara ni kwamba una lima kilimo kinacho kuwezesha kukuza kipato na uchumi wako na uchumi wa Taifa" amesisitiza DED Johnson