Breaking

Wednesday, 17 August 2022

RONALDO AVIVAA VYOMBO VYA HABARI, AVILAUMU KUZUNGUMZA UONGO DHIDI YAKE



Na Said Muhibu,LLH

Mshambuliaji wa Manchester United Christiano Ronaldo amevilaumu vyombo vya habari mbalimbali duniani kwa kuchapisha taarifa zisizo za kweli kumuhusu yeye na mustakabali wake ndani ya klabu yake.

Katika mtandao wa Instagram Ronaldo amesema mara zote vyombo vya habari vimekuwa vikichapicha taarifa za uongo juu yake na kuahidi kuwa wiki chache zijazo atazungumza na vyombo vya habari juu ya mustakabali wake ndani ya klabu ya Manchestar United.

“(Waandishi wa habari) hubaini ukweli pale wanapofanya mahojiano), vyombo vya habari vinazungumza uongo. Nina kijitabu kidogo (ninachokitumia kunukuu taarifa za uongo) miezi iliyopita tabribani taarifa 100 kati ya 5 zilikuwa za uongo, unaweza kufikiria. Lishike hilo,” Ronaldo alichapisha maneno hayo kwenye akaunti yake ya Instagram hapo jana.

Vyombo mbalimbali vya habari vimekuwa vikitofautiana katika kuelezea mustakabali wa Ronaldo ndani ya klabu yake, vyengine husema wakala wa mchezaji huyo Jorge Mendes anatafuta timu nyingine ili mchezaji wake aondoke klabuni hapo na vyingine vikiripoti hakuna timu inayomhitaji Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ureno.

Ronaldo mwenye umri wa miaka 37 amekuwa si mwenye furaha ndani ya klabu ya Manchester United kutokana na mwenendo wake wa kuendelea kupoteza michezo ya ligi kuu tangu ianze kutimua vumbi mnamo agosti 5.

Manchester United ilipoteza mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu ya Uingereza (Premier League) dhidi ya Brighton kwa kufungwa mabao 2-1 mnamo Agosti 7 na kupoteza mchezo wapili dhidi ya Brentford kwa kufungwa mabao 4-0.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages