Maafisa kutoka Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) Nchini Kenya wanachunguza kisa ambapo msichana mmoja wa umri wa miaka 15 aliua ndugu zake wawili na binamu yake.
Kwa mujibu wa DCI, mwanafunzi huyo wa kidato cha kwanza kutoka KAunti ya Kiambu alikiri kutekeleza mauaji hayo katika muda wa mwaka mmoja uliopita.
“Majasusi kutoka Kiambu wanachunguza kisa cha kushangaza ambapo mwanafunzi wa kidato cha kwanza aliua ndugu zake watatu na binamu katika muda wa mwaka mmoja uliopita. Mshukiwa alikiri kuwaua ndugu zake wenye miaka saba, mitano na miwezi 15 kati ya Februari na Julai 2021,” DCI ilisema kupitia kwa taarifa.
Mshukiwa pia alikiri kuwa mwezi jana aliua binamu yake, mtoto wa umri wa miezi 20 kwa kumrusha katika kisimani nyumbani kwao katika kijiji cha Gathiga, kaunti ndogo ya Kabete.
Baba wa msichana huyo wa miaka 15 aliandikisha taarifa katika kituo cha polisi cha Kikuyu.
“Pia alikiri kumuua binamu yake a miezi 20 kwa kumrusha katika kisima nyumbani kwao mwzi jana. Leo babake alielekea katika kituo cha polisi cha Kikuyu na kuandikisha taarifa dhidi ya msichana huyo akimtuhumu kuua wanawe watatu,” taarifa ya DCI ilisema.
Msichana huyo anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Kikuyu akisubiri kufikishwa mahakaman