Breaking

Wednesday, 24 August 2022

AFISA MIPANGO MIJI ADAIWA KUBAKA MTOTO KWENYE GARI



Jeshi la polisi Mkoani Katavi linamshikilia Afisa Mipango Miji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe, Dickson Mwenda mwenye umri wa miaka 37 kwa tuhuma za kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 15 ndani ya gari.

Akithibitisha tukio hilo leo Jumatano August 24, 2022 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi ACP Ali Makame amesema tukio limetokea August 13,2022 saa moja na nusu jioni katika Kijiji na Kata ya Kibaoni Tarafa ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele.

Kamanda Makame amesema Mama wa Mtoto akiwa pamoja na Mtuhumiwa Wakiwa Baa alimkabidhi Mtuhumiwa Mtoto huyo akiwa na Mdogo wake ili awapeleke nyumbani lakini ghafla akiwa njiani aliegesha gari 
(T. 927 DMC) pembeni ya barabara na kumbaka binti huyo.

Tayari Mtuhumiwa amekamatwa na Polisi na kufikishwa Mahakamani katika Mahakama ya Wilaya ya Mlele kujibu tuhuma inayomkabili
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages