Breaking

Wednesday, 13 July 2022

WAZIRI MCHENGERWA KUUNDA KAMATI MAALUM YA KUANDAA MDUNDO MUZIKI WA KITANZANIA




Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema anakwenda kuunda kamati maalum kwa ajili ya kuratibu uzalishaji mdundo wa muziki wa kitanzania ambao utaitangaza Tanzania Duniani.

Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo leo Julai 13, 2022 alipotembelea studio ya kuzalisha kazi za sanaa ya Wanene na kufanya majadiliano na wafanyakazi wa studio hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.

“Dhamira ya Serikali kwa sasa ni kuwa na mdundo utakaoitambulisha nchi yetu kimataifa ili kuuza utamaduni wa nchi yetu kwenye mataifa mbalimbali duniani” amesisitiza Mhe. Mchengerwa.

Amesema Kamati hiyo maalum itaundwa na walimu wabobezi kutoka vyuo vikuu, wazalishaji wa Muziki, wanamuziki pamoja na viongozi wa kimila(machifu).

Amesema Tanzania imebahatika kuwa na utajiri wa utamaduni ambao kama utatumika vizuri kutengeneza midundo ya miziki kama ilivyo kwa nchi mbalimbali duniani utasaidia kuitangaza Tanzania na kuinua uchumi wa Tanzania.

Aidha, amewapongeza wazalishaji hao wa muziki ambapo amesema wanafanya kazi nzuri ya kuandaa kazi bora ambazo zina ubunifu mkubwa.

Amesema amefurahishwa kuona wazalishaji wenye ubunifu mkubwa ambapo amesisistiza kuwa kama watashirikiana kwa pamoja na Serikali wataweza Kwa upande wake Meneja wa Studio ya Wanene Humphrey Domboka amemshukuru Waziri Mchengerwa kwa kuwa karibu na wadau wa wa sekta ambazo anazisimamia.

Domboka amesema endapo Serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi kunakuwa na mapinduzi makubwa ambapo amempongeza Mhe. Rais kwa kazi kubwa anayofanya kwenye sekta ya Sanaa, Utamaduni na Michezo.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages