Breaking

Tuesday, 19 July 2022

WANAFUNZI MBALIMBALI WATEMBELEA BANDA LA DMI KWENYE MAONESHO YA 17 YA ELIMU YA JUU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA

Maafisa usajili kutoka Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) wakitoa elimu na huduma ya usajili kwa wanafunzi waliotembelea banda la Chuo hicho kwenye Maonesho ya 17 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Mhandisi Ibrahim Mpapi akitoa elimu kuhusiana na kozi na fursa zitolewazo na Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kwa mwanafunzi aliyetembelea katika banda la chuo hicho kwenye Maonesho ya 17 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
 Timu ya watumishi kutoka katika Chuo Bahari Dar es Salaam (DMI) katika picha ya pamoja wakiwa tayari kuhudumia wananchi wanaotembelea katika banda lao kwenye Maonesho ya 17 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi waliohudhuria katika ufunguzi wa Maonesho ya 17 ya Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia, yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam . Julai 19, 2022.
 
***********************
 
CHUO cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kimewahimiza wanafunzi waliomaliza Kidato cha Sita kufika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuweza kujisajili na Chuo hicho kwani kumekuwa na fulsa nyingi kwa wale ambao wamekuwa wakijiunga na chuo hicho na kupata elimu ya kutosha kuhusiana na masuala ya bahari.

DMI kupitia timu ya wataalam wao wameendelea kutoa huduma ya usajili wa kozi mbalimbali bila gharama yoyote na kwa haraka na kujihakikishia nafasi ya masomo kwa muda wa masomo unaokuja hivi karibuni.

Akihutubia katika maonesho hayo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa ametoa wito Kwa wazazi na wanafunzi kuja katika viwanja vya Mnazi Mmoja ili kupata taarifa sahihi zinazohusiana na elimu ya juu.

Waziri Mkuu amesema taasisi za elimu ya juu ambazo ni wazalishaji wa maarifa na ujuzi kwa ajili ya maendeleo ya Taifa, hazinabudi kuwa mbele ya wakati siku zote ili kuhakikisha kuwa zinabuni na kuanzisha programu mpya zinazokwenda na wakati.

“Taasisi za Elimu ya Juu na zile za Utafiti na Maendeleo zishirikiane kwa karibu na sekta binafsi, hususan viwanda, na kuweka utaratibu wa kuendeleza teknolojia zinazozalishwa nchini na kuhamasisha matumizi yake ili kuongeza kasi ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi.”

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema kuwa sekta ya elimu ya juu imeendelea kukua kwa kiasi kikubwa kutokana na uwekezaji mkubwa ambao umefanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ikiwa ni pamoja na kushirikiana na sekta binafsi.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages