Breaking

Wednesday, 20 July 2022

UDOM KUTOA FURSA KWA WANAFUNZI



Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Shahada za awali Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Dk Victor George Marealle amesema kuwa mbali na mikopo inayotolewa na bodi ya mkopo lakini pia chuoni hapo kumekuwa na fursa kwa wanafunzi kupata scholer ship mpya ya William Mkapa Foundation ambayo inawasaidia wanafunzi wenye uhitaji lakini ambao wamefaulu vizuri.

Kauli hiyo, ameitoa jijini Dar es Salaam wakati alipokua katika mmaonesho ya 17 ya elimu ya juu Sayansi na Teknolojia wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufunguliwa maonesho hayo na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa.


Amesema kuwa, mbali na fursa ya udhamini kwa taasisi ya Willam Mkapa lakini pia ipo ya Modewji ambayo pia inawataka wanafunzi wenye uhitaji ambao hawana uwezo wa kujilipia ada kuendelea na masomo, hivyo chuo chetu kipo vizuri kumekamilika kila idara mazingira yake yapo vizuri.

Amesema kuwa, chuo chuo kina taasisi mbili, ndaki (colleges)sita, kuna shule kuu tatu ikiwemo ya sheria, shule kuu ya uuguzi na shule kuu ya udaktari, ambapo Chuo hicho ni kikubwa Afrika Mashariki na Kati na kina uwezo wa kuchukua wanafunzi 40,000 na mazingira yake ni mazuri.


"Tuna taasisi ya lugha na taasisi ya taaluma za maendeleo ambayo kwa ujumla tunatengeneza ambazo kwa pamoja tunatengeneza umoja wa taaluma umoja huo unatengeneza shahada za taaluma tofauti tofauti"amesema Dk Marealle.


Aidha, amesema kuna jumla shahada za awali 80 ambazo zimetawanyika katika maeneo ya mbalimbali ikiwemo udaktari, uuguzi, Sayansi asilia, Sheria, Uongozi, Uchumi na Biashara, Tehama na Sayansi ya ardhi pia kuna shahada za juu 53.


"Katika chuo chetu kuna maktaba za kisasa katika kila chuo cha kati ambapo mwanafunzi atapata vitabu vya kutosha na chuo chetu kimejengwa kisasa ambacho kinaweza kuhudumia wanafunzi elfu arobaini katika huduma ya malazi"amesema Dk Marealle.

Hata hivyo, amesema Chuo hicho kiilianza mwaka 2007 ambacho kina wanafunzi 32000 ambao wanasomea fani mbalimbali katika ngazi ya Stashahada, Shahada za awali, Shahada za umahiri na shahada za uzamivu.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages