Breaking

Wednesday, 6 July 2022

TCRA YAWATAKA WAANDISHI WA HABARI ZA MTANDAONI KUTOPOTOSHA JAMII, "ZINGATIENI KANUNI ZA MAUDHUI"

Meneja wa Mamlaka ya Mawasilino Tanzania (TCRA), Mhandisi Francis Mihayo akizungumza katika kikao kazi na Watoa huduma za maudhui kwa njia ya mtandao 'Blogs & Online Tv) Kanda ya Ziwa leo Jumatano Julai 6,2022 katika Ukumbi wa Jengo la TMDA jijini Mwanza.

**************

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewataka waandishi wa habari wa vyombo vya habari za Mtandaoni ikiwemo Blogs na Youtube (Bloggers & Youtubers) kufanya kazi kwa weledi wakizingatia Sheria na Kanuni zinazowaongoza.

Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa, Mhandisi Francis Mihayo ametoa rai hiyo Julai 06, 2022 jijini Mwanza, wakati akifungua kikao kazi baina ya TCRA na waandishi wa habari wa vyombo habari mtandaoni kilicholenga kujengeana uelewa kuhusu mabadiliko madogo ya Kanuni za maudhui mtandaoni.

Mhandisi Mihayo amesema baada ya sekta ya habari mtandaoni kukua hapa nchini, zimeibuka changamoto mbalimbali ikiwemo upotoshaji unaofanywa na baadhi ya runinga za mtandaoni ambapo kichwa cha habari kinakuwa hakina mahusiano na maudhui yaliyo ndani yake.

“Unakuta kichwa cha habari kimeandikwa ‘Imeisha Hiyo’ ukiingia ndani unakuta mwanzo hadi mwisho mtangazaji anasema na neno ‘Subcribe, bonyeza kengele’ kwa habari zaidi, sasa hiyo kwa wataalamu wenye leseni kutoka TCRA sitegemei muwe na kitu kama hicho” amesema Mhandisi Mihayo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza, Edwin Soko akiwasilisha mada kuhusu ulinzi wa waandishi wa habari mtandaoni, amesema wanatakiwa kuimarisha ulinzi wa taarifa na vifaa vyao ikiwemo kutengeneza nywila ili kuepuka kudukuliwa.

“Kuna mambo mbalimbali yanayoashiria vitisho vya kimtandao ambayo mnatakiwa kuwa nayo makini ikiwemo kubonyeza ‘links’ zinazoshawishi kwamba umeshinda zawadi (phishing). Mwaka 2013/15 Facebook na Google walilipa dola milioni 100 kwa watu wasiowahusika baada ya kudukuliwa kutokana na kubonyeza ‘links za aina hiyo” amesema Soko huku akihimiza watumiaji wa mitandao ya kijamii kukinga vifaa vyao kwa kuweka nywila (password) na programu za kupambana na wavamizi mtandaoni (Malware Virus).

Akiwasilisha mada kuhusu maadili ya uandishi wa habari, Mwenyekiti Mstaafu wa MPC Deus Bugaywa amesema changamoto iliyopo kwenye vyombo vya mtandaoni ni kutopitia kwenye dawati la uhariri wa zaidi ya mtu mmoja na hivyo kuwa na makosa mengi ya kimaadili ambapo wengi wa watoa maudhui wamekuwa wakitaka kuwa wa kwanza kutoa maudhui mtandaoni.

Naye Mwanasheria TCRA Joseph Kavishe akiwasilisha mada kuhusu Kanuni za maudhui mtandaoni za mwaka 2022, amesema ni kosa la jinai kuendesha mtandao wa kijamii bila kusajili hivyo kuwasihi bloggers & youtubers kusajili blogs na Online Tv zao ili kuepuka mkono wa sheria huku akiwataka kulinda utu wanapoandika habari zao wakitumia lugha nzuri.

Mamlaka ya Mawasilino Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa imetumia kikao hicho kutoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari mtandaoni kuhusiana na mabadiliko madogo ya Kanuni za Maudhui Mtandao yaliyofanyika mwaka huu 2022 kwa lengo la kuboresha Kanuzi za hapo awali zilizotoka kwa mara ya kwanza mwaka 2018 chini ya Sheria ya EPOCA ya mwaka 2010.

Mabadiliko yaliyofanyika ni pamoja na kupuguza ada ya leseni kutoka shilingi milioni moja hadi shilingi laki tano kwa mwaka na ada ya maombi kutoka shilingi laki moja hadi shilingi elfu hamsini. Lakini pia waandaani wa maudhui yanayohusu michezo, sanaa, mapishi na elimu hawatahitaji kuwa na leseni kutoka TCRA bali leseni hiyo itatolewa kwa wale wanaotoa maudhui ya Habari (News and Current Affairs).

Picha na Kadama Malunde & Samir Salum

Meneja wa Mamlaka ya Mawasilino Tanzania (TCRA), Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati akifungua kikao kazi na Watoa huduma za maudhui kwa njia ya mtandao 'Blogs & Online Tv) Kanda ya Ziwa leo Jumatano Julai 6,2022 katika Ukumbi wa Jengo la TMDA jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa Mwanza Press Club, Edwin Soko akitoa mada kuhusu Vitisho vya Kimtandao na Ulinzi wa waandishi wa habari Mtandaoni kwenye kikao kazi cha TCRA na Watoa huduma za maudhui kwa njia ya mtandao 'Blogs & Online Tv) Kanda ya Ziwa

Mwanasheria TCRA Joseph Kavishe akiwasilisha mada kuhusu Kanuni za maudhui mtandaoni za mwaka 2022 katika kikao kazi na Watoa huduma za maudhui kwa njia ya mtandao 'Blogs & Online Tv) Kanda ya Ziwa leo Jumatano Julai 6,2022 katika Ukumbi wa Jengo la TMDA jijini Mwanza.

Mwenyekiti Mstaafu wa Mwanza Press Club, Deus Bugaywa akitoa mada kuhusu Maadili kwa vyombo vya habari vya mtandaoni
Watoa huduma za maudhui kwa njia ya mtandao 'Blogs & Online Tv) Kanda ya Ziwa wakiwa katika kikao kazi na TCRA Kanda ya Ziwa leo Jumatano Julai 6,2022 katika Ukumbi wa Jengo la TMDA jijini Mwanza.
Watoa huduma za maudhui kwa njia ya mtandao 'Blogs & Online Tv) Kanda ya Ziwa wakiwa ukumbini

Watoa huduma za maudhui kwa njia ya mtandao 'Blogs & Online Tv) Kanda ya Ziwa wakiwa katika kikao kazi TCRA Kanda ya Ziwa leo Jumatano Julai 6,2022 katika Ukumbi wa Jengo la TMDA jijini Mwanza.
Watoa huduma za maudhui kwa njia ya mtandao 'Blogs & Online Tv) Kanda ya Ziwa wakiwa katika kikao kazi na TCRA Kanda ya Ziwa leo Jumatano Julai 6,2022 katika Ukumbi wa Jengo la TMDA jijini Mwanza.
Watoa huduma za maudhui kwa njia ya mtandao 'Blogs & Online Tv) Kanda ya Ziwa wakiwa katika kikao kazi na TCRA Kanda ya Ziwa leo Jumatano Julai 6,2022 katika Ukumbi wa Jengo la TMDA jijini Mwanza.
Watoa huduma za maudhui kwa njia ya mtandao 'Blogs & Online Tv) Kanda ya Ziwa wakiwa ukumbini
Watoa huduma za maudhui kwa njia ya mtandao 'Blogs & Online Tv) Kanda ya Ziwa wakiwa ukumbini
Watoa huduma za maudhui kwa njia ya mtandao 'Blogs & Online Tv) Kanda ya Ziwa wakiwa katika kikao kazi na TCRA Kanda ya Ziwa leo Jumatano Julai 6,2022 katika Ukumbi wa Jengo la TMDA jijini Mwanza.
Watoa huduma za maudhui kwa njia ya mtandao 'Blogs & Online Tv) Kanda ya Ziwa wakiwa katika kikao kazi na TCRA Kanda ya Ziwa leo Jumatano Julai 6,2022 katika Ukumbi wa Jengo la TMDA jijini Mwanza.
Mkutano unaendelea

Watoa huduma za maudhui kwa njia ya mtandao 'Blogs & Online Tv) Kanda ya Ziwa wakiwa katika kikao kazi na Watoa TCRA Kanda ya Ziwa leo Jumatano Julai 6,2022 katika Ukumbi wa Jengo la TMDA jijini Mwanza.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages