Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) kimesema kipo tayari kufanya kazi na wadau wote wakiwemo watafiti, wataalum na wabunifu kwa lengo la kuleta mabadiliko ndani ya jamii, huku kikiahidi kuendelea kufanya kazi kwa ubunifu.
Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Makamo Mkuu wa Chuo hicho, Prof Mohamed Makame Haji wakati akizungumza na waandishi wa habari katika banda lao liliopo kwenye maonesho ya 17 ya elimu ya juu ya Sayansi na Teknolojia ambayo yanaendelea katika viwanja vya mnazi mmoja.
Amesema kuwa, Chuo hicho kinachomilikiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kinaangalia zaidi katika kutoa elimu na kuzalisha rasilimali watu ambao watashiriki kuleta maendeleo ya Taifa, huku akieleza kuwa fani zao zinaangalia zaidi sehemu ambazo vijana wao wataweza kujiajiri pamoja na kutumia vipaji vyao katika kuwekeza kwenye kujiandaa kutengeneza vitu vinavyotokana na ubunifu wao.

Aidha, amesema chuo hicho kinatoa kozi mbalimbali ikiwemo Afya, Ualimu, utalii, fedha, uchumi, biashara, Sayansi jamii, Sayansi asili, Sayansi za bahari pamoja na maeneo mengine kwa upande wa lugha.
Hata hivyo, amesema wanafanya shughuli mbalimbali za kitafiti kwa kushirikiana wataalamu wa ndani na nje ya nchi, vyuo vikuu, Taasisi za elimu na utafiti pamoja na kutoa ushauri elekezi kwa taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi.
Ameongeza kuwa, mkuu wa chuo hicho ambae pia ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi amekuwa akifanya juhudi kuhakikisha chuo hicho kinafanya vizuri, huku akiwekeza nguvu zake zote kuhakikisha chuo kinatoa huduma katika mazingira mazuri na kujenga maadili mema.
Sambamba na hayo amesema SUZA inaangalia sera kuu za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuhamasisha lugha ya kiswahili kwa wageni kwa kutumia wataalamu wa ndani na nje ikiwemo kutoa elimu kwa wageni.
"Katika kukuza kiswahili tunatoa fani za kitaalam na zisizo za kitaalam ambazo ni za elimu za kiswahili kuanzia ngazi ya cheti, hadi nngazi ya Shahada ya uamivu (PhD), hii yote namna bora ya kukuza lugha ya kiswahili na kupata mafuaa makubwa ulimwenguni"amesema Prof Makame.
Ameongeza kuwa, wana kituo maalum ambacho kinaangalia namna bora ya uboreshaji wa lugha ya kiswali ambapo wanafanya tafiti na kuwakusanya wataalamu kwa kufanya makongamano, kutayarisha vitabu na vitini vinavyotumika kufundishia lugha ya kiswali Ili kuhakisha kinafika mbali zaidi.