Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema ametoa agizo hilo wakati wa kikao maalumu Cha baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini Kilichokuwa Kinajadili Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali kikao Ambacho kilikuwa na jumla ya hoja 104 Ikiwa hoja 53 zikiwa ni Mpya zilizoibuliwa na (CAG) na hoja Mpya 51 zikiwa ni hoja za Miaka ya nyuma.
Rc Mjema amesema Halmashauri ya Shinyanga vijijini kupitia Baraza lake la Madiwani linapaswa kuhakikisha kila mara linasimamia vyema fedha zote ambazo zinatolewa kwa ajili ya shughuli za Miradi ili kuepuka mrundikano wa hoja ambazo zinaibuliwa na na (CAG).
Amesema lengo sio Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali anapoibua hoja kwa Halmashauri basi wanakuwa wa kutupiana lawama badala ya kukutana mara moja na kuanza kushughulikia ili kuanza kuzijibu na kuzitatua.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga vijijini Nice Munissy amesema kikao hicho kimekuwa na mafanikio baada ya kuweza kupata ufafanuzi toka kwenye hoja mbalimbali ambazo ziliibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali hivyo kusababisha hoja nyingi kupata ufafanuzi kwa haraka.
Ameongeza kuwa Mwaka huu wa fedha wameweza kupata hati Safi na hiyo ndiyo lengo ambalo Halmashauri hiyo imejiwekea kusimamia vyema na kudhibiti upotevu wa fedha ambazo zinatolewa kwa ajili ya maendeleo .