Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan leo Julai 05, 2022 amekutana Timu ya Mpira wa Miguu ya Wanawake chini ya Umri wa Miaka 17 ( Serengeti Girls) Ikulu Dar es Salaam na kuipongeza kwa kufuzu kucheza Kombe la Dunia nchini India.
Mhe. Rais, pia amewapongeza viongozi wakuu wa Wizara ya Utamaduni kwa ubunifu wao ambao umeleta mapinduzi makubwa na kusisitiza kuwa ushirikiano wao ni jambo ambalo limesaidia kutapa matokeo chanya katika sekta wanazozisimamia.
Katika hafla hiyo ambayo Mhe. Rais aliwakaribisha rasmi kwenye chakula cha mchana na kuwapa zawadi, amewataka wachezaji hao kujiandaa vema kuelekea katika mashindano ya dunia huku akisisitiza kufanya mazoezi na kuzingatia lishe.
Hafla hiyo, imepambwa na Wasanii wa Muziki wa kizazi kipya akiwemo Barnaba na Frida Amani ambao waliotumbuiza kwa jumbe nzuri zilizowa
Naye Mhe. Mchengerwa amesema mafanikio ya kufuzu kwa Timu hiyo yamechagizwa na maono, maelekezo, utashi na dhamira ya ukweli ya kuweka juhudi za dhati katika kuwekeza na kuwezesha rasilimali katika shughuli za michezo ambazo amezifanya Mhe. Rais.
Amesema ndani ya mwaka mmoja aliridhia asilimia 5 ya mapato ya Fedha za Michezo ya Kubashiri Matokeo ya michezo (Sports Betting), kuwa ni moja ya chanzo cha kudumu cha mapato ya kutunisha mfuko wa maendeleo ya michezo nchini.
Amefafanua kuwa fedha hizo zimesaidia timu mbili kufuzu kushiriki Kombe la Dunia ambazo ni Serengeti Girls na timu ya Taifa ya mpira wa miguu kwa watu wenye ulemavu (Tembo worriers).
Aidha, fedha hizi zimeanza kuifanya Tanzania kuwa kitovu (hub) ya michezo hapa Afrika kwani zimewezesha kuandaa (Host) mashindano makubwa ya kimataifa hapa nchini ya mchezo wa mpira wa miguu kwa watu wenye ulemavu Afrika (CANAF,2021,) ambapo nchi 12 za Afrika zilishiriki; Mashindano ya Afrika ya Mchezo wa Kabadi ambapo nchi tano (5) za Afrika zilishiriki ikiwemo Misri; Mashindano ya Afrika Mashariki ya Ngumi za Ridhaa, Mashindano ya Bara la Afrika ya Mchezo wa Baseball (Afrika Baseball -5), Mashindano ya Afrika ya Mchezo wa Mpira wa Mikono (Handball), na Mashindano ya Mpira wa Kikapu ya Afrika (Basketball Zone 5).
Ameongeza kuwa fedha hizi zimeleta manufaa ya kimkakati ambapo zimerejesha hamasa ya michezo kwa kina mama ambapo mwaka jana lilianzaliwa Tamasha kubwa la Michezo kwa wanawake (Tanzanite Women Sports Festival)
“Mhe. Rais zimesaidia kurejesha matumaini ya vijana wengi wenye vipaji vya michezo mbalimbali wa mikoani wasioonekana ambapo mwaka jana zikarejesha Mashindano ya Taifa Cup yaliyoshirikisha vipaji kutoka mikoa karibu yote.
Amesema mambo haya makubwa mwaka huu wanatarajia kuyaboresha zaidi kupitia programu ya Mtaa kwa Mtaa hadi Taifa Cup” amesisitiza Mhe Mchengerwa.
Aidha, amesema fedha hizo zimeanza kuwa mkombozi ambapo amefafanua japo haziwezi kutosha kwa kila kitu, lakini zimeiwezesha Wizara kupitia BMT kufadhili Timu mbalimbali za Taifa ikiwemo kuigharamia Serengeti Girls kwa posho zao, safari na malazi.