Breaking

Sunday, 3 July 2022

NAULI ZA MELI NEW MV VICTORIA, NEW MV BUTIAMA ZAPANDA, KUANZA KUTUMIKA KESHO JULAI 04



Na Samir Salum, Lango la habari

Gharama za nauli ya kusafiri kwa njia ya maji kati ya miji ya Mwanza na Bukoba kwa meli ya New Mv Victoria "Hapa Kazi Tu"  Na New Mv Butiama "Hapa Kazi Tu" inayoelekea Nansio imepanda kwa wastani wa Sh2, 445 hadi Sh10, 000 kwa safari.

Kwa mujibu wa Afisa Masoko Mkuu Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) Eugenia Punjila amesema bei mpya zitaanza kutumika kuanzia Julai 4, 2022 huku akieleza kuwa mabadiliko hayo yametokana na kupanda kwa gharama za uendeshaji.

Punjila amesema kuwa nauli za daraja uchumi iliyokuwa Sh16, 000 kwa mtu mzima imepanda hadi Sh21, 000 huku nauli ya watoto ikipanda kutoka Sh8, 550 hadi Sh11, 000.

Kwa abiria wanaosafiri katika daraja la biashara ambao awali walilipa nauli ya Sh30, 000 sasa watalipa Sh40, 000 huku kwa watoto ikiwa ni shilingi elfu 21.

Wazazi watakaosafiri na watoto wao katika daraja hilo sasa watawalipia nauli ya Sh21, 000 badala ya Sh15, 550 ya awali, ikiwa ni ongezeko la Sh5, 450 kwa safari.

Nauli za daraja la kwanza iliyokuwa Sh45, 000  imeongezeka hadi kufikia Sh55, 000 huku watoto ambao awali walilipiwa Sh23, 050 sasa watalipiwa Sh26, 000.

Kwa upande wa New Mv Butiama Bunjila amesema kuwa kwa daraja la kwanza (Biashara) nauli imeongezeka kutoka sh10,000 kwa watu wazima hadi kufikia Sh 12,000 huku kwa watoto ikiwa ni Sh 7,000.

"Daraja la Pili (Uchumi) ilikuwa ni Shilingi Elfu 8 kwa watu wazima sasa ni Elfu 10 huku kwa watoto ikiwa ni elfu 6." Amesema Punjila

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages