Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma linamshikilia Mwalimu wa Shule ya Msingi Nyamgeni Wilayani Uvinza Asafu Lutebuka(30) kwa tuhuma za kumbaka na kumsababishia ujauzito Mwanafunzi wake wa darasa la sita mwenye umri wa miaka 16 kinyume cha sheria.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Ramadhan Kingai amesema Mtuhumiwa huyo alikuwa akimpeleka Mwanafunzi wake nyuma ya kichaka jirani na Shule hiyo kila baada ya masomo ya jioni na kufanya nae mapenzi na kwamba akikataa kesho yake anamchapa viboko.
Kamanda Kinghai amesema kuwa baada ya wazazi wa mwanafunzi huyo kuona Mtoto wao akiwa katika hali isiyo ya kawaida walienda kumpima na kugundulika kwamba alikua na mimba ya mwezi mmoja na nusu.
"Binti huyo alihojiwa juu ya ujauzito huo ndipo alimtaja mwalimu huyo kuwa ndie aliyekua akifanya vitendo hivyo na Mwanafunzi wake" ameeleza Kamanda Kinghai
Kamanda Kighai amesema Mtuhumiwa huyo atafikishwa Mahakamani mara baada ya taratibu za upelelezi kukamilika.