Polisi katika Kaunti ya Homa Bay wanamzuilia mwanamke mmoja kwa tuhuma za kumdunga na kumuua mumewe wakati wa mzozo kuhusu simu katika baa moja mjini Homa Bay Nchini Kenya.
Mwanamke huyo alimuua mumewe kwa kumdunga kwa kisu wakiburudika katika baa.
Mshukiwa alitiwa mbaroni Siku ya Jumatano Julai 13, 2022 mchana baada ya kumdunga mwanamume mwenye umri wa miaka 31 aliyetambulia kama Charles Okoth Onyango wakati wakibugia mvinyo.
Onyango alikuwa wa Serikali katika kaunti ya Hombay na alifariki eneo la tukio baada ya kujeruhiwa vibaya kufuani.
Kwa mujibu wa walioshuhudia, Onyango alifika kwenye baa hiyo na kuagiza vinywaji ambavyo alifurahia pekee yake akiwa kwenye kona ya baada hiyo, lakini baadaye mwanamke mmoja, anayetajwa kuwa mkewe, akajiunga naye na kuanza kubugia mvinyo vilevile.
Wawili hao walipokuwa wanaendelea kunywa vyao, mzozo ulizuka kati yao.
Inadaiwa mshukiwa aliomba simu ya Onyango kusoma meseji ambazo alikuwa akipokea.
Onyango anaripotiwa kukatalia simu yake na badala yake kuanza kumkosoa mshukiwa kwa kumuuliza maswali na kilichooanza kama mazungumzo kati ya wapenzi kikatokea kuwa mzozo mkubwa na kuvutia masikio ya watu wengine.
Mzozo huo ulipofika kilele chake, mwanamke huyo alichomoa kisu na kumdunga Onyango kifuani.
Alikuwa amebeba kisu hicho katika kibeti chake kwa kile kinachooneka kuwa alikuwa amejiandaa kuua.
Kwa mujibu wa chifu wa kata ya Homa Bay mjini Joshua Ochogo, mshukiwa alimdunga mwendazake mara moja kabla ya kuanguka na kuaga dunia.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa kaunti ndogo ya Homa Bay Sammy Koskeyi, uchunguzi katika kisa hicho unaendela huku mwili wa marehemu ukipelekwa katika makafani ya Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Homa Bay.