Breaking

Thursday 28 July 2022

MAPINDUZI FC YAICHAPA MBAO FC 1-0 MICHUANO YA UTALII CUP 2022




TIMU ya Mapinduzi FC ya Mwanza leo Alhamisi Julai 28, 2022 imeifundisha adabu timu kongwe ya Mbao FC katika mchezo wa pili wa Utalii Cup 2022 uliochezwa katika uwanja wa Nyamagana Mwanza.

Katika mchezo huo uliokuwa na mnyukano wa kutosha, timu ya Mapinduzi iliuteka mchezo kwa kucheza na spidi na maarifa makubwa zaidi ya Mbao FC.

Dakika ya arobaini na mbili Mchezaji wa Mapinduzi FC Alphonse Sospeter alifunga goli la timu hiyo akimalizia kazi iliyofanywa na Khalfan Salum na kuitanguliza Mapinduzi FC kwa goli 1-0.

Hadi Mapumziko Mapinduzi walikuwa mbele kwa goli 1-0 na kipindi cha pili Mbao FC walipambana kutafuta kusawazisha bao hilo ili ikashindikana. Hadi dakika tisini goli likabaki kuwa 1-0.

Ikumbukwe Jumatano 27 Julai mwaka huu ndio Michuano hiyo ilianza kwa timu ya Alliance FC kucheza na Copco FC na Copco FC kupata ushindi wa magoli 3-0.

Baada ya mechi hiii yanafuatia mapumziko hadi tarehe 1 Agosti mwaka ambapo itapigwa mechi ya tatu baina ya Pamba FC wakicheza na Jendele FC kutoka Zanzibar Saa 10 Jioni katika uwanja wa Nyamagana Mwanza.

Michuano hii inaandaliwa na Fraki Co LTD na kusimamiwa na Chama cha Soka Mkoa wa Mwanza MZFA, lengo likiwa kuhamasisha Utalii katika michezo na kufungua fursa mbalimbali katika Utalii.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages