WAZIRI MKUU kassim majaliwa amewasisitiza viongozi wa vyama vya siasa kutumia majukwaa yao pamoja na masuala mengine ya kisiasa, wakemee biashara na matumizi ya dawa za kulevya.
Ameyasema hayo Jumamosi, Julai 02, 2022 wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupinga Matumizi ya Dawa za Kulevya yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar Es Salaam.
Majaliwa amesema wanasiasa hawana budi kutumia vikao na mikutano yao katika kupinga matumizi ya dawa za kulevya. “Tumieni vikao vyenu vya ngazi mbalimbali pamoja na mikutano ya hadhara kuunga mkono Serikali katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya.”
Amesema viongozi wa dini wanapotekeleza jukumu lao la kutoa mafundisho ya kiroho na kukemea dhambi na uovu pia, wawekeni msisitizo katika kukemea dawa za kulevya kwani huo ni uhalifu kama ulivyo uhalifu wa aina nyingine.
Kwa upande wa wanahabari, Waziri Mkuu amewataka watumie vyombo vyao vya habari kuendelea kukemea matumizi na biashara ya dawa za kulevya. Kwa upande mwingine toeni habari kwa umma kuhusu huduma zinazotolewa kwa waathirika wa dawa za kulevya.
“Serikali yetu inafanya mambo makubwa sana tangazeni ili Wananchi wote waweze kufahamu na kwa wale walioathirika waweze kutumia huduma zinazotolewa na hatimaye wapate tiba kamili na kuendelea kuchangia nguvu kazi ya taifa letu.”
Aidha, Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwaasa wazazi na walezi na jamii kwa ujumla kuwalea watoto katika misingi ya maadili ili kuwaepusha na vitendo viovu ikiwemo matumizi na biashara haramu ya dawa za kulevya.

“Turejee kwenye asili yetu ambapo jamii nzima ilihusika katika malezi ya watoto na ilishirikiana katika kukemea maovu.”
Kaulimbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu inasema “Tukabiliane na Changamoto za Dawa za Kulevya kwa Ustawi wa Jamii”.