Breaking

Monday, 18 July 2022

KANISA LA AICT TANZANIA LAADHIMISHA MIAKA 80 YA UMISIONARI YA AIM (AFRICA INLAND MISSIONARY)



Kanisa la AICT Tanzania wameadhimisha miaka 80 ya utumishi wa Umishonari wa Africana Inland Missionary) katika kanisa hilo, ambayo yamefanyika katika AIC Tanzania Pastoreti ya Butundwe, kanisa la pamoja la Nyasembe.

Maadhimisho hayo yameongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la AICT Tanzania Mussa Masanja Mwagwesela, maaskofu, wachungaji, wainjilisti, viongozi wa Kiserikali, kwaya mbalimbali na waumini wa kanisa na wengine kutoka maeneo mbalimbali.

Mwakilishi wa African Inland Missionary Mchungaji Andrew Andersen amesema kipindi huduma ya Umisioonari unaanza lengo likiwa ni kusaidia kujenga makanisani na kusukuma maendeleo ya eneo husika ambalo makanisa hayo yalionzishwa.

Akizungumza kuhusiana na Umisionari wa eneo la Nyasembe Butundwe, Askofu Mkuu AICT Tanzania Mwagwesela amesema maadhimisho hayo yamebeba maudhui ya kuendeleza kile ambacho kilianzishwa na kuboreshwa yaliyoanzishwa.

Mbunge wa jimbo la Busanda Mhandisi Tumaini Magesa amesema wao kama wawakilishiwa wananchi wanashukuru yote yaliyofanywa na Wamisionari hao wa AIM (African Inland Missionary).

Kwa niaba ya Maaskofu, wachungaji na wainjilisti walioashiriki katika maadhimisho hayo wamesema wamefurahishwa na kile walichokifanya Wamisionari wa AIM na kuomba waendelee kusapoti maendeleo nchini Tanzania.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages