Breaking

Wednesday, 20 July 2022

HALI YA BARIDI KUFIKIA 4°C MBEYA, NJOMBE NA IRINGA




Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), imesema kwamba hali ya baridi itaendelea kuwepo ambapo katika mikoa ya Njombe, Iringa na Mbeya baridi inatarajiwa kufikia viwango vya chini vya nyuzi joto 4°C.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mtaalam wa uchambuzi wa hali ya hewa kutoka TMA Rose Senyagwa, amesema hali ya mvua zinazonyesha ni za nje ya msimu ambapo zimetokana na hewa kunyonya unyevunyevu baharini na hivyo kupelekea mvua hizo kunyesha.

Kuhusu hali ya barafu iliyojitokeza hivi karibuni mkoani Njombe, Senyagwa amesema hali hiyo inayofahamaika kama Sikitu inatokana na majimaji ya unyevunyevu kuganda na hivyo kupelekea barafu hizo hali ambayo ni kawaida kunapokuwepo na baridi kalI

Source: EATV
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages