Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu Bwa. Kaspar Mmuya amesema uboreshwaji wa huduma zinazotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Wakala wa Biashara na Leseni (BRELA) zitasaidia wananchi kupata huduma mbalimbali na wawekezaji kuwekeza kwa wingi Nchini.
Naibu Katibu Mkuu huyo ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati wa kikao cha Makatibu na Wakuu wa Taasisi kujadili utekelezaji wa Mkataba wa Huduma kati ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Wakala wa Biashara na Leseni (BRELA).
Amesema kutatuliwa kwa changamoto zinazokabili mamlaka hizo kunatoa fursa kwa wafanyabiashara kuanzisha bishara zao, viwanda kwa mujibu wa sheria hivyo kuongeza pato la mtu mmoja mmoja hadi Taifa kwa ujumla.
###MWISHO###