Na Lucas Raphael,Tabora
Mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Nzega mkoani Tabora imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela Masanja shija(58) baada ya kupatikana hatia ya kufanya mapenzi na mtoto wake wa kike aliyekuwa chini ya miaka 18.
Akitoa hukumu hiyo jana hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama ya wilaya ya Nzega,Godfey Rwekite alisema kutokana na ushahidi kukamilika mahakamani hapo imeridhia kumuhukumu Masanja Shija kutumikia kifungo hicho cha miaka 30 jela.
Alisema adhabu hiyo iwe fundisho kwake na kwa watu wengine wenye tabia kama hizo za kufanya vitendo vya ukatili kwa watoto hususani watoto wao wa kike.
Awali mawakili wa serikali kutoka ofisi ya taifa ya mashitaka walipo wilayani nzega wakiongozwa na Jenipher Mandago. Waliiambia mahakama hiyo kuwa kesi hiyo ni ya jinai namba 90/2021 mnamo desemba 2 mwaka 2021 majira ya usiku Masanja Shija alifumaniwa akifanya mapenzi na mtoto wake wa kike mwenye umri chini ya miaka 18.
Wakili huyo wa serikali waliongeza kwa kusema kutokana na ushahidi kukamilika mahakamani hapo waliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa Masanja Shija ili iwe fundisho kwake na kwa watu wengine wenye nia ovyo na wanaoendekeza vitendo vya kikatili katika wilaya ya nzega.
kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo mshitakiwa Masanja Shija alipewa nafasi ya kujitetea ambapo aliomba kupunguziwa adhabu kutokana nakuwa na familia inayomtegemea.
hata hivyo mahakama hiyo haikuridhia na utetezi wake hivyo mahakama chini ya hakimu Godfrey Rwekite ikamuhukumu Masanja Shija kutumikia kifungo hicho cha miaka 30 kwa kosa la kufanya mapenzi na mtoto wake wa kike.
Mwisho.