Breaking

Wednesday, 15 June 2022

YANGA SC YATWAA UBINGWA WA LIGI KUU 2021/22


KLABU ya Yanga imefanikiwa kunyakuwa ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara mara baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya timu ya Coastal Union.


Yanga Sc ilikuwa inahitaji pointi tatu ambazo zingeifanya isifikiwe na timu yoyote ile kwa michezo iliyosalia ya kigi kuu ya NBC.


Mabao ya Yanga yamewekwa kimyani na mshambuliaji wao Fiston Kalala Mayele ambaye alipachika mabao mawili katika dakika ya 34 na 67 na bao lingine likifungwa na Chiko Ushindi katika dakika ya 51.


Mayele sasa ataendelea kuongoza ufungaji bora akiwa na mabao 16 akifuatia na mshambuliaji wa Geita Gold George Mpole.


Timu ya Yanga sasa imefikisha ubingwa wa ligi kuu mara ya 28 tangu kuchkua ubingwa huo 2016/2017.


Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages