Wizara ya Madini kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Canada imeanza maandalizi ya kushiriki katika Maonesho Makubwa ya Madini yanayohusisha Wazalishaji na Watumiaji wa Bidhaa zinazohusisha Madini Duniani ( PDAC), yanayotarajiwa kufanyika nchini humo.
Ujumbe wa Tanzania katika Maonesho hayo unahusisha Wizara ya Madini na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) ambapo wizara inatarajiwa kunadi fursa zake za kiuwekezaji zilizopo katika Sekta ya Madini kwa wawekezaji duniani.
Kwa mara ya kwanza Bara la Afrika limepewa kipaumbele kutangaza fursa zake za kiuwekezaji katika maonesho hayo.
Aidha, pamoja na kuonesha fursa hizo, Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko anatarajiwa kutoa mada kuhusu fursa za uwekezaji zilipo kwenye Sekta ya Madini katika eneo la utafutaji madini ya aina mbalimbali, uchimbaji , uchenjuaji, biashara ya Madini pamoja na shughuli za kutoa huduma kwenye migodi ya Tanzania.
Hatua hiyo inalenga kuongeza uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya Madini.