Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amekutana na msanii nguli kutoka Nigeria Jim Iyke na kufanya mazungumzo ya mashirikiano katika kuandaa filamu za kimkakati za pamoja baina ya Tanzania na Nigeria
Mazungumzo haya yamefanyika leo Juni 14, 2022 jijini Dodoma ambapo wamekubaliana kuwa na mashirikiano kwenye filamu za kimkakati kwa faida za pande zote mbili.
Waziri Mchengerwa amesema mashirikiano hayo yataifanya Tanzania kunufaika zaidi kwa kufanya kazi na manguli wa filamu wa Nigeria ambao wanawapenzi wengi duniani.
Ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wadau mbalimbali duniani kuja kuwekeza kwenye sekta ya Sanaa na Michezo.
Ameongeza kuwa kwa sasa tayari imeshusha kodi ya zuio katika biashara ya filamu kutoka asilimia 15 hadi 10 ili kuyapa unafuu makampuni yanayofanya masuala ya filamu nchini.