Breaking

Thursday, 16 June 2022

WATUMISHI WIZARA YA MADINI WAADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

 



Wizara ya Madini inaungana na Watanzania wote nchini kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma inayofanyika kuanzia Juni 16 mpaka 23 ya kila mwaka ambapo wizara hiyo inafanya maadhimisho hayo katika ofisi zilizopo Mji wa Serikali Mtumba.


Maadhisho hayo, yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji wa hiari kwa watumishi wa umma, kusikiliza changamoto zinazowakabili kiutendaji na kupokea maoni mbalimbali ya watumishi wa umma.

Maadhimisho hayo ya mwaka 2022 yamebebwa na kauli mbiu isemayo “Kuimarisha Ustahimilivu wa Utawala wa Umma katika Afrika ili kuwezesha utambuzi wa mahitaji ya lishe Afrika wakati na baada ya Janga la Covid-19”.


Kufuatia hatua hiyo, watumishi wa Wizara ya Madini na wadau mbalimbali wanaendelea kutembelea maadhimisho hayo ambapo kila mmoja ametoa maoni na changamoto zinazo wakabili katika utendaji wao wa kazi. 


Pamoja na mambo mengine, Wizara ya Madini inawakaribisha watumishi, wadau wa Sekta ya Madini na watanzania kwa ujumla kutembelea madhimisho yanayoendelea katika Ofisi za wizara hiyo jijini Dodoma.












Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages