Breaking

Tuesday, 7 June 2022

WATU WATANO WAFARIKI DUNIA, 12 WAJERUHIWA AJALI YA TRENI NA LORI - KENYA


Na Samir Salum, Lango La Habari

Watu watano wamefariki dunia na wengine 12 kujeruhiwa baada ya treni kugongana na lori huko Ruiru, Kaunti ya Kiambu Nchini Kenya.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari kamanda wa polisi wa Kaunti ya Kiambu, Muchangi Kioi amesema kuwa ajali hiyo imetokea Jana Jumatatu Juni 06, 2022 jioni katika Daraja la Reli la Kihunguro.

Kamamda Kioi amesema dereva wa lori lori hilo ambalo ni la Kampuni ya Utengenezaji wa Uchina lilikuwa likisafirisha vibarua kutoka kazini alikuwa akiendesha mwendo wa kasi ili kuwahi treni inayokuja na kusababisha ajali hiyo.

Amedai kuwa abiria waliokuwa kwenye roli walijaribu kuruka nje ya lori lililokuwa likienda kasi lakini haikuwezekana hali iliyosababisha watu watano kufa huku wengine 12 wakiuguza majeraha mabaya na wanapokea matibabu katika hospitali mbalimbali za Kaunti ya Kiambu.

“Miili minne ilipatikana ikiwa imenasa chini ya treni. Mwathiriwa mmoja alifariki wakati wa matibabu hospitalini, huku wengine 12 wakiendelea kupata nafuu,”

"Tutaendelea kufuatilia hali ya wale ambao bado wanapata matibabu katika hospitali mbalimbali lakini tunataka kuwaonya wananchi kukaribia maeneo ya reli kwa tahadhari. Ni afadhali kusimama na kusubiri treni ipite badala ya kuwa na matukio kama haya," amesema Kamanda Kioi

Shirika la Reli la Kenya lilitoa taarifa yake Jana kwenye ukurasa wake wa Twitter kuaa treni hiyo ilikuwa ikisafirisha matandiko matupu ilipata ajali kwa kugonga lori ambalo lilikwama lilipokuwa likijaribu kuvuka njia ya reli kwenye kivuko kisicho halali.

"katika eneo la tukio na waliojeruhiwa wamekimbizwa hospitalini,” imesema taarifa ya shirika la reli la Kenya.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages