Watu 9 wamekamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Kigoma,kwa tuhuma za kukutwa na viungo vinavyodhaniwa ni vya binadamu ikiwemo mbavu na mguu wakisafirisha kupeleka kwa mtu aliyepo katika kijiji cha Nyehungwe,wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza
Kamanda wa polisi mkoani Kigoma James Manyama amesema watu hao walikamatwa May 30 katika Kijiji cha Kanyonza wilaya ya Kakonko baada ya kuzuiwa na polisi katika kuzuizi,walikamatwa wakiwa kwenye gari namba T 948 DQU aina ya Pro Box wakipeleka kwa mteja aliyekuwa akihitaji viungo.
“Mtuhumiwa mmoja alimtaja mtu mmoja (jina linahifadhiwa) aliyekuwa akimpelekea viungo hivyo Sengerema, Mwanza, baada ya kufuatiliwa walikamatwa.”