Mkuu wa Mkoa wa Geita Bi.Rosemary Staki Senyamule akiambatana na Kamati ya ulinzi ya usalama ya Wilaya ya Nyang'hwale katika ziara yake wilayani humo amesikitishwa na kitendo cha baadhi ya watu waliokatisha Maisha ya Watoto wawili mmoja miaka 7 na mwingine miaka miwili kwa kuchinjwa kikatili hadi kufa wilayani humo.
Akizungumza mbele ya Mkutano wa hadhara alioufanya na wananchi katika eneo hilo Bi.Senyamule ameliagiza Jeshi la Polisi Mkoani humo kuhakikisha wanakamatwa wote na kufikishwa katika vyombo vya kisheria huku akiwataka waganga wa kienyeji wenye ramli chonganishi kuhama mara moja kabla kuwachukulia hatua.
Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa Geita Kamishina Msaidizi Henry Mwaibambe amesema chanzo cha matukio hayo ni kuhusishwa na imani za kishirikina baina ya Familia na Familia.
Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa Geita Kamishina Msaidizi Henry Mwaibambe amesema chanzo cha matukio hayo ni kuhusishwa na imani za kishirikina baina ya Familia na Familia.
Kamanda Mwaibambe amesema tayari baadhi ya watuhumiwa wamekwisha kufikishwa katika vyombo vya sheria kwa ajili ya kuhojiwa huku akiwataka wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la polisi kuwafichua watuhumiwa hao.