Breaking

Wednesday, 29 June 2022

WATARKIOSK YASHIRIKI JUKWAA LA UWEKEZAJI WA UMEME VIJIJINI


Mkurugenzi mtendaji na Mwanzilishi wa Boreal Light na Waterkiosi Dkt. Hamed Behest ( wa kwanza Katikati) akimpatia maelezo kuhusu Waterkiosi Balozi wa EU Nchini Tanzania, Manifredo alipotembelea banda la WatarKiosk kwenywe Jukwaa la Uwekezaji la Umeme Vijijini la Alliance for Rural Electricity (ARE) la Uwekezaji wa Upatikanaji wa Nishati 2022 jijini Dar es Salaam, Tanzania, kuanzia tarehe 28-30 Juni.
Balozi wa EU Nchini Tanzania, Manifred akitazama moja ya mradi wa kusafisha maji uliofanywa na Waterkiosi alipotembelea banda lao kwenye Jukwaa la Uwekezaji la Umeme Vijijini la Alliance for Rural Electricity (ARE) la Uwekezaji wa Upatikanaji wa Nishati 2022 jijini Dar es Salaam, Tanzania, kuanzia tarehe 28-30 Juni.
Mkurugenzi mtendaji na Mwanzilishi wa Boreal Light na Waterkiosi Dkt. Hamed Behest (Wa Kwanza kushoto), na Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Kampuni ya WatarKiosk , Samuel Kinyanjui (Katikati) wakizungumza na moja ya mdau alipotembelea banda lao kwenye kwenywe Jukwaa la Uwekezaji la Umeme Vijijini la Alliance for Rural Electricity (ARE) la Uwekezaji wa Upatikanaji wa Nishati 2022 jijini Dar es Salaam, Tanzania, kuanzia tarehe 28-30 Juni.
Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Kampuni ya WatarKiosk , Samuel Kinyanjui akimpatia maelezo Maandishi wa habari kuhusu mashine ya kusafisha maji ambayo inatumia miale ya jua wakati wa Jukwaa la Uwekezaji la Umeme Vijijini la Alliance for Rural Electricity (ARE) la Uwekezaji wa Upatikanaji wa Nishati 2022 jijini Dar es Salaam, Tanzania, kuanzia tarehe 28-30 Juni.

PICHA ZOTE NA YUSUPH DIGOSSI- SAUTI ZA MTAA BLOG
*******************************************


Kampuni ya WatarKiosk ambayo inamiliki mtambo wa kusafisha maji safi kwaajili ya kunywa na matumizi ya Kilimo imeshiriki Jukwaa la Uwekezaji la Umeme Vijijini la Alliance for Rural Electricity (ARE) la Uwekezaji wa Upatikanaji wa Nishati 2022 jijini Dar es Salaam, Tanzania, kuanzia tarehe 28-30 Juni.


Katika Jukwaa hilo wawakilishi kutoka sekta za umma na binafsi, ikiwa ni pamoja na WatarKiosk, wanakutana kama sehemu ya shughuli zinazoendelea , Waziri wa Nishati Tanzania , January Makamba na Balozi wa EU Manifredo walikua wageni rasmi.


Akizungumza na waandishi wa habari ambao walitembelea banda la WatarKiosk , Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo , Samuel Kinyanjui mtambo huo una uwezo wa kusafisha Lita Elfu Ishirini (20,000) kwa siku za maji ya habari, ya kisima au maji ya aina yoyote.


Amesema mtambo huo unatumia miale ya jua ' Solar Energy' ambapo yanapitishwa katika mtambo huo na kutoa chembechembe za uchafu na kupita kwenye chemba Maalumu ambayo inachuja chumvi na kutoa maji safi na salama kwaajili ya kunywa na matumizi ya Kilimo.


Amesema mradi huo unasaidia jamii kwa kuwapa huduma ya maji safi kwa gharama pia wanatoa huduma hiyo katika hospitali kwaajili ya wagonjwa na wafanyakazi wa vituo vya afya.


Amesema kwa Tanzania mradi huo unatoa huduma Kibaha Mkoa wa Pwani, Zanzibar na Afrika Mashariki huduma hiyo inapatikana Nchini Kenya.


Naye Mkurugenzi mtendaji na Mwanzilishi wa Boreal Light na Waterkiosi Dkt. Hamed Behest amesema kuwa Mkutano huo utaongeza fursa ya kujenga ushirikiano kati ya Kampuni yao na wadau kutoka mataifa mbalimbali ambao wamehudhuria Mkutano huo.


Kuhusu utunzaji wa Mazingira Mkurugenzi huyo amesema kuwa mashine ya WatarKiosk haichafui mazingira kwasababu inatumia mfumo wa nishati ya jua .


" Sisi hatuchafua mazingira hatuchomi mkaa, hatutumii mafuta , hivyo tunatoa wito kwa wadau kutumia nishati mbadala ili kuendelea kutunza mazingira ya dunia"amesema Dkt. Behesti.


Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages