Breaking

Wednesday, 1 June 2022

WATALII ZAIDI YA 50 KUKWEA MLIMA KILMANJARO KWA BAISKELI


Na Edmund Salaho, KILIMANJARO


Zaidi ya Watalii 50 ambao pia ni wanamichezo wa baiskeli kutoka mataifa mbalimbali duniani leo wameianza safari yao ya  mashindano kukwekwea Mlima Kilimanjaro kwa baiskeli umbali wa zaidi ya mita 5895 kutoka usawa wa bahari.

Mashindano hayo yaliyodhaminiwa na taasisi ya Grumeti Fund maarufu kama “Kilimanjaro2Natron” ikiwa na lengo la kujionea mandhari na uzuri wa nchi ya Tanzania. 


Akizungumza katika ufunguzi wa mashindano hayo Mkuu wa Idara ya Utalii, Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro, Afisa Uhifadhi Mwandamizi, Charles Ngendo alisema


“Tukio hili ni fursa kubwa kwa Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro ambapo leo tumepokea zaidi ya wageni 50 ambao ni wanamichezo wa baiskeli maarufu duniani kutoka mataifa mbalimbali wenye wafuasi wengi katika mitandao ya kijamii na kama hifadhi tunatumia fursa hii kujitangaza, kuongeza idadi ya wageni na kuongeza mapato kwa serikali yetu”


Aidha, Mhifadhi Ngendo ametoa rai kwa watanzania hususani vyama vya waendesha baiskeli nchini kuja kufanya mchezo huo katika hii kwani inawezekana kufanya mashindano  katika mlima huo.  


Kwa upande wake meneja wa taasisi ya Grumeti Fund ambao ni wadhamini wa mashindano haya, Matty Perry aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa kukubali ombi la kufanya mashindano hayo kwenye Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro.

“Tunashuruku wenzetu wa TANAPA na Serikali ya Tanzania kwa ujumla kwa kutoa kibali kwa ajili ya mashindano haya kwani hakuna mashindano kama haya katika nchi zingine.  Kwa kweli mashindano haya ni ya kipekee sana” alisema Perry


Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro ina mazao mbalimbali ya utalii kama Kuruka kwa parachuti, kupanda Mlima Kilimanjaro kwa kutembea pamoja na utalii wa kupanda miamba ya kilele cha Mawenzi.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages