Viongozi 7 wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wanatarajiwa kukutana leo Juni 20, 2022 Jijini Nairobi, Kenya mada kuu ikiwa ni mgogoro unaoendelea kati ya DRC na Rwanda.Mkutano huo unakuja wakati kumezuka mapigano makali yanayofufua uhasama wa miongo kadhaa kati ya Congo na Rwanda, huku DRC ikiilaumu Rwanda kutokana na kuibuka upya hivi karibuni kwa kundi la Waasi la M23.
Rwanda imekanusha mara kwa mara kuwaunga mkono Waasi hao huku nchi zote mbili zikilaumiana kwa kufanya mashambulizi ya kuvuka mpaka.
Ofisi ya Rais wa Kenya imesema Watu wa mashariki mwa DRC wameteseka kwa muda mrefu na wanaendelea kulipa gharama kubwa kupita kiasi kwa kupoteza maisha, mali na amani.
Siku ya Jumatano, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alitoa wito wa kutumwa mashariki mwa DRC kikosi cha kikanda ili kurejesha amani lakini Congo ilisema haitakubali kamwe ushiriki wa Rwanda katika operesheni hiyo.