Na Ayoub Julius,Lango la habari
Vincent Kompany atakuwa na jukumu la kuinoa Burnley kurejea Ligi Kuu baada ya kumrithi Sean Dyche kama meneja wao wa kudumu.
Nahodha wa zamani wa Manchester City Vincent Kompany amethibitishwa kuwa meneja mpya wa klabu ya Burnley baada ya kuondoka Anderlecht.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 alitumia miaka mitatu kuinoa Anderlecht kama meneja wachezaji, kabla ya kujiuzulu kwa makubaliano mwezi uliopita.
Anachukua mikoba ya Turf Moor kabla ya msimu wa kwanza wa Burnley katika Ligi ya Mabingwa tangu 2015-16 kufuatia kushushwa daraja kutoka Ligi kuu ya Uingereza.
Sean Dyche alifutwa kazi na Burnley mwezi Aprili baada ya kuiongoza kwa muongo mmoja, huku bosi wa muda Mike Jackson akishindwa kuiweka klabu hiyo kwenye ligi kuu.
Burnley walithibitisha uteuzi huo kwenye tovuti yao rasmi Jumanne, ingawa hawakutangaza urefu wa mkataba uliotiwa saini na Mbelgiji huyo.