Na Said Muhibu, Lango la habari
Timu ya Taifa ya wanawake Twiga stars imeiangushia mvua ya magoli 12-0 dhidi ya timu ya taifa ya Zanzibar kwenye mchezo wa michuano ya Shirikisho la vyama vya soka Afrika Mashariki na kati (CECAFA) ya wanawake 2022 inayoendelea nchini Uganda.
Ushindi huo wa kishindo umeifanya Twiga stars kutinga hatua ya nusu fainali ambapo itakutana na timu ya taifa ya Burundi mnamo Alhamis June 9, 2022.
Mchezo huo ulianza kwa Twiga stars kupata goli la mapema dakika ya 7' lililofungwa na Oppa Clement na kufuatiwa na mvua ya magoli 5-0 yaliyohitimisha kipindi cha kwanza, huku wachezaji Janeth Pangamwene, Diana Msewa, Enekia Lunyamila wakiwa wamezitikisa nyavu ya timu ya taifa ya Zanzibar, Oppa Clement akiingia nyavuni mara mbili
Kipindi cha pili hakikuwapa matumaini yoyote Zanzibar kwani Twiga stars waliendeleza kichapo hadi mchezo huo kutamatika kwa mabao 12-0. Mabao ya kipindi cha pili yalifungwa na Mwanahamis Omar akiingia nyavuni mara tatu, Protas Mbunda, Opa Clement akiingia nyavuni mara mbili na Ester Mabanza.
Aidha, wachezaji wa Twiga stars Oppa Clement na Mwanahamis Omar wameibuka nyota wa mchezo kwa kuondoka na mpira, timu ya taifa Twiga stars imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ambapo itacheza dhidi ya timu ya taifa ya Burundi mnamo Alhamis June 9, 2022.