Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema kuwa Tanzania na India zinakwenda kupitia na kuboresha mikataba ya mashirikiano ya awali kwenye eneo la Utamaduni na Sanaa iliyojiwekea mwaka 1984 ili kuiboresha iweze kuleta mapinduzi makubwa na ya haraka kwa faida ya pande zote.
Mhe, Mchengerwa ameyasema haya leo Juni 17, 2022 akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Hassan Abbasi wakati alipotembelewa ofisini kwake na Balozi wa India nchini Mhe. Binaya Srikanta Pradhan na kufanya mazungumzo ya kuendeleza mashirikiano kwenye sekta hizo.
Aidha, amesema mambo mengi yalikubalika baina ya nchi zote mbili hususan kuendelea kwa tamaduni pia kumekuwa na mambo mengi ambayo yameandikwa ambayo kuna haja ya kufanya mapitio.
Ameongeza kuwa katika maongezi hao wamekubaliana kuwa na kituo maalum cha kuandaa filamu ambacho kitatumika kwa nchi za Afrika mashariki ambapo baadhi ya wasanii kutoka India watashiriki moja kwa moja kwenye eneo hili.
Pia amesema eneo jingine kubwa ambalo wamejadili ni kuhusu umuhimu wa wa kufanya mkutano mkubwa kuhusu bahari ya Hindi ambao utajumuisha nchi hizo mbili.
Amesema tamasha hilo litasaidia kuonyesha historia za nchi zote zilikotoka zilipo na zinakoelekea
Aidha, amesema bahari ya Hindi imebeba historia kubwa ambayo tayari watafiti kutokana India na Tanzania wamefanya utafiti hivyo ni muhimu kuutumia utafiti huo kwa faida ya nchi zote.
Naye Mtaalam na Mtafiti Arindam Mukherjee ambaye ameambatana na Mhe. Balozi amefafanua kuwa tafiti zinaonesha kuwa Bahari ya Hindi ilikuws ikitumika kwa miaka mingi kufanya biashara ambapo yapo baadhi ya maeneo ambayo yamethibitika yamekuwa yakikaliwa na waswahili na pia kumekuwa na mfanano wa maneno ya kiswahili.