Breaking

Wednesday, 8 June 2022

TANZANIA KUPATIWA MSAADA WA DOLA MILIONI 25 NA WAFADHILI WA GFF


PARIS, UFARANSA

Tanzania kupatiwa msaada wa dola milioni 25  sawa na shilingi bilioni 57 za Kitanzania kutoka kwa wafadhili wa afya ya mama na mtoto (GFF) kwa ajili ya kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto nchini.


Hayo yamebainishwa leo kwenye Mkutano wa 14 wa  Global Financing Facility For Women, Children and Adolescent Health (GFF) ambapo Tanzania inawakilishwa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu jijini Paris,Ufaransa.


Waziri Ummy amesema kuwa Tanzania GFF mwaka 2015/2016 ilitoa msaada kama huo kwa ajili ya afya ya mama na mtoto kiasi cha shilingi bilioni 40.


Waziri Ummy amekiambia kikao hicho kuwa Tanzania imepiga hatua katika utoaji wa hufuma za mama na mtoto na zipo dalili ya kupungua kwa vifo vitokanavyo na uzazi na watoto.


"Tanzania ina historia ndefu ya huduma za afya za msingi,Serikali zote zilizopita hususani Mhe.Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Awamu ya nne ya Jamhuri ya Tanzania aliweka mkazo mkubwa kwenye huduma za afya ya msingi".Alisema.


Hata hivyo Waziri Ummy amesema  kuwa bado Tanzania ina kazi kubwa ya kufanya ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya na kwa wakati hivyo amewaomba wafadhili hao kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania.


"Tunawaomba tuendelee kushirikiana ili kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto katika kipindi hiki ambacho Tanzania inajivunia kuwa na Rais wa kwanza Mwanamke Mhe. Samia Suluhu Hassan.


Mkutano wa 14  wa wafadhili wa Afya ya Mama na Mtoto unafanyika jijini hapa kuanzia tarehe 6 hadi 8 Juni, 2022 ni mkutano muhimu wa wadau katika ustawi wa Sekta ya Afya na unajadili masuala mbalimbali ikiwemo uimarishwaji wa huduma za afya katika ngazi ya msingi.


Vilevile kikao hiki kinajadili changamoto zilizopo na mafanikio yaliyopatikana kupitia ufadhili wa GFF pamoja na namna bora ya kuongeza rasilimali watu kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ikiwemo kuwapatia mafunzo mahususi watumishi wa afya na kuwaongezea vitendea kazi ili kuboresha huduma zinazotolewa kwenye vituo vya afya ngazi ya msingi.


-Mwisho-




Mkutano huu wa wadau muhimu katika ustawi wa Sekta ya Afya unajadili masuala mbalimbali ikiwemo uimarishwaji wa huduma za afya katika ngazi ya msingi ambapo kikao hiki kinajadili changamoto zilizopo na mafanikio yaliyopatikana kupitia ufadhili wa GFF. Aidha, wajumbe wa kikao hiki wanajadili namna bora ya kuongeza rasilimali watu kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ikiwemo kuwapatia mafunzo mahususi watumishi wa Afya na kuwaongezea vitendea kazi ili hatimaye kuboresha huduma zinazotolewa kwenye vituo vya afya ngazi ya msingi. 


Kikao hiki pia kinajadili suala la upatikanaji wa rasilimali fedha na namna bora ya kusimamia fedha zinazotolewa na Wafadhili mbalimbali ili kuhakikisha kuwa yanapatikana matokeo chanya zaidi yaliyokusudiwa katika kusukuma ajenda ya kuimarishaji huduma za afya ngazi ya msingi.


Kwa upande wake Mhe. Ummy amekiambia kikao hiki kuwa Tanzania ina historia ndefu ya huduma za afya za msingi. Serikali zote zilizopita hususani ya Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Awamu ya 4 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliweka mkazo mkubwa kwenye huduma za afya za msingi. Kupitia huduma hizi, Tanzania imepiga hatua katika utoaji wa huduma za mama na mtoto, na kuna dalili ya kupungua kwa vifo vitokanavyo na uzazi na watoto. Hata hivyo Mhe Ummy amesema kuwa bado Tanzania ina kazi kubwa ya kufanya hususani kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za Afya na kwa wakati. Hivyo amewaomba wafadhili hao kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania ili kuboresha huduma za Afya ya Mama na Mtoto hususani katika kipindi hiki ambacho Tanzania inajivunia kuwa na Rais wa kwanza Mwanamke mama Samia Suluhu Hassan.


Mwaka 2015/16 GFF imetoa msaada kwa Tanzania kiasi cha dola milioni 40 (takribani shilingi bilioni 92) kwa ajili ya Afya ya mama na  mtoto. Na sasa GFF wataipatia Tanzania msaada wa dola milioni 25 (kiasi cha shilingi bilioni 57) kwa ajili ya kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages