Breaking

Sunday, 19 June 2022

TAASISI YA MWANAMKE INITIATIVE YAPONGEZWA KUSAIDIA MTOTO WA KIKE ZANZIBAR


Wadau mbalimbali wa kupigania maendeleo ya mtoto wa kike nchini wamejitokeza  kuchangia takribani  shilingi  bilioni moja  kwenye  taasisi ya Mwanamke Initiative Foundation (MIF) inayojishughulisha na kumkwamua mtoto wa kike katika elimu ili kutimiza ndoto zake. 


 Wadau hao wametoa michango  hiyo katika  halfa maalum ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na taasisi ya hiyo usiku wa kuamkia leo Juni 19, 2022 Zanzibar  na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa ambaye ni mume wa Wanu.

Taasisi hiyo inatarajiwa kuzinduliwa Rasmi leo Jumapili Juni 19, 2022 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.


Akizungumza katika hafla hiyo Mwenyekiti na Mwanzilishi wa Mfuko huo, Wanu Ameir ambaye pia ni Mbunge wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar na mtetezi wa haki  za vijana na wanawake amewashukuru wadau mbalimbali waliojitokeza na amewaomba kuendelea  kuchangia ili kuwasaidia Watoto wa kike  waweze kutimiza ndoto zao.


 “Naomba kuchukua  fursa hii kushukuru sana isiwe mwanzo wala mwisho naomba iwe mwanzo na tuendelee kuchangia  mfuko wetu wa Mwanamke Initiative ili kuona kwamba mtoto wa kike anasimama  na anaweza kushindana katika ulimwengu” amefafanua.

Wakitoa maoni yao kwa nyakati tofauti tofauti kuhusu kuanzishwa kwa mfuko huo, wamepongeza jitihada kubwa zinazofanywa na MIF kwa kuwasaidia watoto wa kike Zanzibar huku wakitoa rai kwa wadau wengi zaidi  kushiriki kwenye jitihada hizo za kuwakomboa Watoto wa kike kwa kuchangia kwa hali na mali katika mfuko huo ili lengo liweze kutimia. 


“Tumefarijika sana na kazi kubwa na nzuri zinazofanywa na mfuko huu, tunaomba na wadau wengine waendelee kujitokeza kuchangia kwa  kuwa ukimsaidia mtoto wa kike aweze kujikwamua umesaidia taifa”aliongeza Tuli Mwambapa ambaye ni Mkurugenzi wa Benki ya CRDB nchini.

Benki ya CRDB ni moja kati ya wadau waliochangia ambapo imetoa kiasi cha shilingi milioni mia tatu.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages