Ubalozi wa Tanzania Nchini Malawi umesema kuwa Serikali ya Malawi imesitisha kuuzwa kwa Mahindi nje ya nchi kutokana na mashaka ya kuwa na upungufu wa chakula.
Taarifa hiyo imetolewa leo Jumatatu Juni 20,2022 na Balozi wa Tanzania Nchini Malawi Humphrey Polepole kwenda kwa wafanyabiashara wa mazao ya wa Tanzania.Balozi Polepole amesema Ubalozi wa Tanzania nchini Malawi unafuatilia suala hili kwa karibu huku ukiwataka Wafanyabiashara kusitisha mpango wa kununua mahindi nchini malawi mpaka Ubalozi utakapotoa taarifa nyingine.