Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Mtwara na TAKUKURU kuhakikisha wanafuatilia na kuwachukulia hatua baadhi ya Watumishi wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoani humo ambao wamekuwa sio waadilifu na kuwanyanyasa Wafanyabiashara kwa kuwafungia biashara zao.
Shaka ameyasema hayo katika kikao cha majumuisho ya ziara yake ya siku nne Mkoani Mtwara.
"Mkuu wa Mkoa huko TRA kuna mambo inabidi mkayaangaliee, Rais alipoingia madarakani jambo moja kubwa alilolifanya ni kufungua uchumi wa nchi, kuna biashara zilifungiwa Rais alipoingia zikafunguliwa"
"Kuna Watu wanafungia Watu biashara lakini TAKUKURU tusaidieni mkitaka tuwasaidie tutawapa baadhi ya Watumishi wa TRA vitendo wanavyofanya haviendani na maadili ya kazi zao"
"Kumekuwa na wimbi la kufunga biashara za Watu kwa makosa madogomadogo ambayo hayana msingi hatuwezi kuona dhamira njema ya Rais inakwamishwa baadhi ya Watu wanataka kumkwamisha Rais Samia"