Na Samir Salum, Lango la habari
Mamia ya wapenzi wa burudani Mkoani Mwanza wamejitokeza katika usiku wa tukio la uchekeshaji liliofanyika katika ukumbi wa New Mwanza Hotel usiku wa kuamkia leo Jumapili Juni 12, 2022.
Tukio hilo lililoandaliwa na Jukwaa la Rock City Comedy limepambwa na wachekeshaji mbalimbali wakiwemo Osmond Soka, Amos Comic, Matilda, Sam Comedian, Mbwana Jamal na Tinno huku Mshairi, Mr Romantic Akisherehesha katika Usiku huo.
Akizungumza mara baada ya tukio hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Rock City Comedy, Julius Muniko amesema kuwa kuanzishwa kwa Jukwaa hilo ni kutoa fursa kwa vijana kuonesha vijapi vyao na kuwawezesha kujikwamua kiuchumi.
Muniko amesema wapo vijana ambao kupitia kikundi hicho wameweza kukuza zaidi vipaji vyao na kupata fursa za kiuchumi katika Warsha mbalimbali hivyo amewaasa vijana wenye kipaji cha kichekesha kujiunga na kikundi hicho.
Awali Mmoja wa Wachekeshaji, Osmond Soka ameishukuru Rock City Comedy kuwa moja ya sehemu iliyomfanya kuwa mshindi wa tatu katika mashindano ya vipaji kwa wanavyuo ya Uni Tarent 2022 na kuondoka na Fedha Taslim Shilingi Milioni Moja.
Aidha , Soka amewaomba wadau mbalimbali pamoja na Serikali kujitokeza kudhamini Jukwaa la Rock City Comedy ili kuwawezesha kuendesha Matukio mbalimbali kwa ajili ya kutoa Burudani na kukuza fursa za kiuchumi kwa vijana wanaojiunga na Jukwaa hilo.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Baadhi ya wadau waliohudhuria Jukwaa la Rock City Comedy lililofanyika Usiku wa kuamkia leo Juni 12, 2022 New Mwanza Hotel.(Picha Zote na Samir Salum, Lango la habari )
Cheko si haba ndani ya Jukwaa la Rock City Comedy lililofanyika Usiku wa kuamkia leo Juni 12, 2022 New Mwanza Hotel.
Baadhi ya wadau waliohudhuria Jukwaa la Rock City Comedy lililofanyika Usiku wa kuamkia leo Juni 12, 2022 New Mwanza Hotel.
Mchekeshaji Sawe boy Akiwasha moto katika Jukwaa la Rock City Comedy lililofanyika Usiku wa kuamkia leo Juni 12, 2022 New Mwanza Hotel.
Mchekeshaji Akiwasha moto katika Jukwaa la Rock City Comedy lililofanyika Usiku wa kuamkia leo Juni 12, 2022 New Mwanza Hotel.
Baadhi ya Wadau waliojitokeza katika Jukwaa la Rock City Comedy lililofanyika Usiku wa kuamkia leo Juni 12, 2022 New Mwanza Hotel.
Mshairi Mr Romantic akisherehesha katika Jukwaa la Rock City Comedy lililofanyika Usiku wa kuamkia leo Juni 12, 2022 New Mwanza Hotel.
Mshairi Mr Romantic akitumbuiza katika Jukwaa la Rock City Comedy lililofanyika Usiku wa kuamkia leo Juni 12, 2022 New Mwanza Hotel.
Mchekeshaji Amos Comic Akiwasha moto katika Jukwaa la Rock City Comedy lililofanyika Usiku wa kuamkia leo Juni 12, 2022 New Mwanza Hotel
Mchekeshaji Akiwasha moto katika Jukwaa la Rock City Comedy lililofanyika Usiku wa kuamkia leo Juni 12, 2022 New Mwanza Hotel
Baadhi ya Wadau waliojitokeza katika Jukwaa la Rock City Comedy lililofanyika Usiku wa kuamkia leo Juni 12, 2022 New Mwanza Hotel.
Mchekeshaji Sam Comedian Akiwasha moto katika Jukwaa la Rock City Comedy lililofanyika Usiku wa kuamkia leo Juni 12, 2022 New Mwanza Hotel.
Mchekeshaji Osmond Soka aliyekuwa Mshindi wa tatu katika mashindano ya vipaji kwa wanavyuo ya Uni Tarent 2022 Akiwasha moto katika Jukwaa la Rock City Comedy lililofanyika Usiku wa kuamkia leo Juni 12, 2022 New Mwanza Hotel
Picha Zote na Samir Salum, Lango la habari