Breaking

Thursday, 30 June 2022

RC MJEMA AWATAKA MADIWANI KUHOJI MATUMIZI YA FEDHA ZA MIRADI MANISPAA YA KAHAMA




Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Sophia Mjema amewataka Madiwani katika Halmashauri ya Manispaa Kahama kutosita kuhoji pale watakapobaini dosari yoyote katika maendeleo au fedha za Miradi zisipo tumika ipasavyo.

Rc Mjema ametoa wito huo leo Alhamisi Juni 30, 2022 wakati wa kikao maalumu Cha baraza la Madiwani cha kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali kikao hicho ambacho kilikuwa na jumla ya hoja 87 huku kukiwa na hoja 60 ambazo Manispaa hiyo tayari imezifanyia kazi na kufungwa na jumla ya hoja 27 bado utekelezwaji wake unaendelea.


Amesema Manispaa hiyo ya Kahama imejitahidi katika kupunguza wingi wa hoja ambazo zilipelekea kuwa na Idadi ndogo ya hoja tofauti ambazo ziliwasilishwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali huku akitoa agizo la kuhakikisha ifikapo tarehe 15/07/2022 hoja zote zinazopaswa kushughulikiwa ziwe zimetatuliwa na kufungwa.

Aidha ameongeza kuwa endapo Madiwani wasipokuwa makini katika kuhoji matumizi ya fedha zote ambazo zinatolewa na Serikali wataisababishia Manispaa hiyo kuwa kwenye mtiririko wa hoja nyingi na baadae kupelekea kupata hati chafu.

"' Nawapongeza Madiwani kwa kuwa makini katika kuhoji matumizi sahihi ya fedha zote ndani ya Manispaa yenu sawa mara kwa mara mnapata hati Safi Sasa muendelee hivyo hivyo na mjitahidi kusiwepo na hoja kabisa" amesema Rc Mjema


Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga amesema Manispaa ya Kahama imekuwa ni Moja ya Manispaa katika Mkoa wa Shinyanga ambayo ina vyanzo vingi vya mapato na jukumu walilonalo ni kuhakikisha wanasimamia vyema vyanzo vyote vya mapato ili kutotegemea fedha nyingi toka serikali Kuu.

Naye Mkurugenzi Halmashauri ya Manispaa Kahama Bwn. Anderson D.Msumba amesema Manispaa hiyo imejipanga kuhakikisha inatekeleza maoni na ushauri uliotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2020/2021
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages