Mkuu wa mkoa akiwa na maafisa wa TRA
Meneja wa Songwe wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Dickson KimaroAfisa uhusiano Mkuu Bw. MacDonald MwakasindileMkuu wa Mkoa wa Songwe Bw. Omari Mgumba akizungumza mara baada ya kukutana na Maafisa wa Mamlaka wa TRA.
***************
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Bw. Omari Mgumba akutana na Maafisa wa Mamlaka wa Mapato TRA na kuishukuru Mamlaka hio kwa kuwatembelea walipakodi hao wa Mkoa wa songwe kwa ajili ya kutoa elimu mlango kwa mlango kufanya hivo itapelekea uelewa mpana kwa wafanyabiashara wa Songwe kujua wajibu wa mamlaka na wajibu wakulipakodi.
Pia Mkuu wa mkoa aliendelea kwa kusema wafanyabiashara hao kutoa ushirikiano wa dhati kwa ajili ya kupata elimu ya kodi, kwakuhakikisha wasanimamia maneno na maelekezo ya Serikali ya Mh. Raisi wa Tanzania Samia Suluhu Hassan bila kutumia nguvu, bila kutumia mabavu na bila kutumia hila, Mamlaka ya Mapato imekua ikikusanya kodi kwa weledi kukutana na wafanyabiashara kuwapa elimu ili kujua umuhimu wa kodi na madhara ya ukwepaji kodi.
Vilevile alitoa rai kwa wafanyabiashra wanapouza bidhaa watoe risiti na mnunuzi kudai risiti kwa kutokufanya hivo nikuikosesha mamlaka na serikali mapato yake halali na kudhoofisha juhudi za serikali.
Kwa upande wa Meneja wa Songwe wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Dickson Kimaro aliongezea kwa kusema ujio wa Maafisa hao kutoka Makao makuu utasaidia ongezeko la ukusanyaji wa mapato nakuondoa changamoto walizokua nazo walipakodi katika mkoa huo wa Songwe.
Nae pia Afisa uhusiano Mkuu Bw. MacDonald Mwakasindile kutoka Makao Makuu TRA amesema kuwa kuwa zoezi hili linafahamika kwa jina la mlango kwa mlango linalenga kuwahudumia wafanyabiashara ili kuangalia jinsi wanavyolipa kodi.