Na Lydia Lugakila, Kagera
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi Mkoani Kagera kusimamia vyema fedha za ujenzi wa miradi ya maendeleo kwa malengo yaliyokusudiwa.
Rais Samia ametoa maagizo hayo leo Juni 08, 2022 wakati akizungumza na wananchi wilayani Biharamulo ikiwa ni katika ziara ya siku 3 Mkoani Kagera.
Amesema kuwa fedha nyingi zimekusanywa na zitaendelea kuletwa kwa wananchi hivyo hakuna haja ya kukaa nazo au kuona zinatuna kwenye mifuko bure hivyo ni vyema viongozi walioaminiwa wasimamie vyema miradi mbali mbali ya maendeleo inayotolewa na serikali kwa malengo husika.
" Kwa maneno ya mkuu wa Mkoa ,wakuu wa wilaya na wabunge simamieni vyema fedha hizo kwa matumizi lengwa"alisema Rais Samia.
Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Jenerali amempongeza Rais Samia kwa namna anavyowajali wananchi katika kufanikisha miradi mbali mbali ya maendeleo.